Header Ads

Eti! Jike Shupa Afunguka mazito Haogopi NgomaHAMNAZO! Msanii muuza sura katika video za Bongo Fleva, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai haogopi Ukimwi kwa kuwa ni ugonjwa wa kawaida, ndiyo maana amekuwa akibadili wanaume ovyo bila wasiwasi.
Aliiambia safu ya Za Motomoto News kuwa wanaume wengi wamekuwa wakimtokea na kumhitaji kimapenzi, hivyo kutokana na uwingi wao, anajikuta akishindwa kuwakatalia wote hivyo kuwakubalia, pamoja na ukweli kuwa humpa fedha.

“Sioni shida kubadili wanaume kila siku maana wao wenyewe ndiyo wanaonitamani, siogopi Ukimwi maana kila mtu duniani ameathirika, huo ni ugonjwa wa kawaida kama mwingine, wanaume wanaonitamani ni wengi hivyo nashindwa kuwakataa,  naingia nao kwenye uhusiano siku mbili tatu tunaachana, nakuwa na mwingine,” alisema Jike Shupa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.