Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Kimenukaa...Mwigulu Awapa 'Makavu Live' Jeshi la Polisi Nchini...!!!

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amewataka maafisa wa jeshi hilo kutenda haki kutokana na baadhi yao kunyooshewa vidole kwa kukiuka misingi ya kazi zao ikiwamo kujihusisha na rushwa.
Waziri Nchemba pia amelitaka jeshi hilo kuhakikisha linaendelea na mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwamo vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya huku akiahidi dhamira ya serikali katika kuongeza maslahi ya askari polisi nchini pamoja na miundombinu ya makazi yao. 
Ametoa agizo hilo katika kikao cha kazi kilichoongozwa na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu na kuhudhuriwa na maafisa waandamizi, makamanda wa mikoa na wakuu wa vikosi vya polisi nchi nzima ambapo pamoja na mambo mengine kinajadili mikakati ya kukabiliana na uhalifu nchini. 
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Waziri Nchemba amesema serikali itaendeleza jitihada zake za kuwakomboa askari katika kuongeza maslahi yao pamoja na kuboresha miundombinu ya askari
Kwa upande wake mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu amesema mapambano dhidi ya madawa ya kulevya imekuwa ni tatizo sugu nchini na kuitaka jamii kutofumbia macho vitendo hivyo vya kihalifu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.