Header Ads

Mrembo Diana Afunguka Dhuluma Aliyofanyiwa Miss World 2016 na Mkenya...


Hii ndiyo story nzima ya Miss world 2016.
Katika mashindano yale hawaangali urembo tu bali na lengo la Urembo yaani (BeautyWithaPurpose) na hivyo kila mshiriki anatakiwa atengeneze ya kwake ,hivyo mimi niliamua kutengeneza ya tofauti kidogo maana ni ngumu kupata video ya mtu anayekeketwa nikaamua kuonyesha kwa njia ya documentary , nikaiupload youtube mnamo tarehe 18 October 2016 kwa mara yakwanza na baadaye kuongeza baadhi ya maudhui katika ile documentary ya kwanza hii ilikuwa kwaajili ya maandalizi ya kwenda missworld, na baada ya hapo nikaipost tarehe 24 November 2016 .Nilipofika Washington nilikabidhi CD na pia tuliituma kwa njia ya email kwenda Miss World. Baada ya hapo tukaitwa usiku mmoja na tukaambiwa tunaoneshwa documentary zilizofanya vizuri na yangu iliingia kwenye 24 bora na ikasifiwa sana lakini siku baada ya kuoneshwa kesho yake asubuhi alikuja Miss Ghana katika chumba changu akiwa na hasira sana nkaamuuliza nini shida akasema Miss kenya anamuudhi ,na hapo kwa ajili hasira akaniambia Miss kenya kaenda kukushtaki kwa Mkuu wa MissWorld kuwa BWP yako hujaitengenezea nchini kwenu na yake ina maudhui mengi kuliko yangu.Nilipomjulisha Meneja hakutaka kuamini kuwa Taasisi kubwa kama Miss World haiwezi kuaminishwa kwa maneno ya mdomoni bila kufanya uchunguzi wa kina,lakini baada ya hapo muaandaji wa miss Kenya alikuwa ameshafika na akawa analalamika sana eti kwanini miss Kenya hafanyi vizuri akawa anashauriana naye vitu vingi.Baadaye tukatajiwa Top5 Kenya ikaingia ile hali haikuwepo katika orodha ya 24 Bora japo kwa kipindi chote hicho alikuwa hajaonesha documentary siku tulipotakiwa tukionesha documentary zetu.

Muandaaji wa Miss kenya alikuja wiki mbili kabla ya fainali na alikuwepo kwenye group la whatsapp la Miss world ambalo kimsingi lilikuwa ni group mahususi kwaajili ya washiriki tu na baadaye alijisahau akatuma meseji kumuuliza Evelyn kwanini havai hereni zenye kuitambulisha Kenya.Swali linakuja je alifuata nini kwenye group na aliingizwaje kwenye group la washiriki ambalo lilikuwa linajumuisha na viongozi wa MissWorld.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.