Header Ads

Rasmi..Diamond Aamua Kumchana Makonda Ukweli wa Moyo Wake..!!!

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva,  Nasib Abdul ‘Daimond Platnumz’, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda kwa jitihada zake kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa salama.
“Kwanza kabisa Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda kwa jitihada zake. Ukizingatia ni mwaka mmoja tu tokea awe mkuu wa mkoa lakini utendaji wake umezaa matunda mengi na changamoto ni nyingi zinazo mkabili lakini bado amekuwa imara.”, alisema Diamond.
Diamond ameyasema hayo leo katika mkutano  kuhusu vita dhidi ya madawa ya kulevya uliofanyika katika Bwalo la Polisi Oster Bay jijini Dar es Salaam ambako Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na viongozi wengine wa serikali na taasisi mbalimbali walihudhuria.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.