Header Ads

VideoFUPI: Mtangazi wa Clouds TV kanyolewa nywele katika kipindi, aliahidi atafanya hivyo Arsenal ikitolewaMoja kati ya watu waliyowashangaza mashabiki wengi wa soka wiki moja iliyopita ni huyu mtangazaji wa Clouds TV James Tupatupa ambaye pia ni shabiki wa Arsenal ya England, Tupatupa aliahidi kama Arsenal itatolewa na FC Bayern Munich atanyoa upara.
Ahadi hiyo James Tupatupa aliitoa baada ya Arsenal kufungwa goli 5-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliyochezwa katika uwanja wa Allianz Arena mjini Munich Ujerumani, hivyo mchezo wa marudiano Tupatupa alikuwa na imani Arsenal yake itaishangaza dunia.
Kwa bahati mbaya Arsenal imetolewa kwa kufungwa kipigo kama cha mwanzo cha goli 5-1 na kuondolewa kwa jumla ya kufungwa goli 10-2, hivyo kutokana na ahadi yake Tupatupa ambaye anapenda kukaa na Afro na hapendi kunyoa alilazimika kutekeleza ahadi yake katika kipindi cha Clouds 360.

ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.