Header Ads

Watanzania Ni Watu wa Ajabu Sana!, Wanamwaminije Gwajima Kuliko Rais Wako?!.

Ni ukweli usiofichika watu wana mwamini zaidi Mchungaji Gwajima na uongo wake kuliko wanavyo mwamini rais wao na ukweli kumhusu mteule wake.
Kuna ule msemo usemao "you can fool some people for sometimes but you can't fool all the people all the time" ukimaanisha unaweza kuwadanga baadhi tuu ya watu kwa wakati fulani au kwa muda fulani tuu lakini huwezi kuwadanganya watu wote na kwa wakati wote au mara zote na siku zote, lakini Watanzania ni watu wa ajabu kweli, unaweza kuwadanganya wote na wakati wote! .
Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza hili swali "how does it come the same people wanachaguliwa katika chaguzi mbalimbali kwa kuja na ahadi kem kem, mwisho wa siku, wanashindwa kuzitekeleza, na bado wanawarudia na ahadi nyingine kem kem na mnawachagua tena? . Yaani wanawadanganya all the people all the time na bado tunawachagua?. Kipindi cha uchaguzi niliwahi kuuliza swali hili, sikupata majibu ya kuridhisha.
Hii kadhia ya Mkuu wetu wa Mkoa kusingiziwa uongo, imenifundisha kitu. Watanzania ni watu wa ajabu sana, ni warahisi kudanganyika na wepesi wa kusahau.
Juzi kati Mchungaji Gwajima aliibuka na uongo wa mchana kweupe na kumsingizia Makonda ameiba jina la Paul Christian, na ameghushi vyeti vya Paul Christian kujifanya ndio yeye na akafoji kuvitumia kusomea chuo kikuu na kupata ajira ukiwemo uteuzi wa rais wa JMT kuwa DC na sasa ni RC. Mchungaji Gwajima akadai kuwa jina halisi la Makonda ni Daudi Albert Bashite. Uongo huo haukuishia hapo bali alidai kuwa anavyo vyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha alipata Division 0 na pia anavyo vyeti vya Paul Christian ambavyo Daudi Bashite aliviiba na kuvitumia kama vyake. 
Baadhi ya sisi wenye imani haba, kama Tomato tulionyesha kutomwamini Mchungaji Gwajima kwa kumuita ni muongo hadi pale atakapoonyesha hivyo vyeti tuvione ndipo tuamini. 
Kitu cha ajabu sana Watanzania wengi wamemwani Gwajima, hivyo sio tuu kumtaka Makonda aonyeshe vyeti vyake bali hadi kushinikiza ajiuzulu au atumbuliwe! . Ajiuzulu kwa kosa lipi au atumbuliwe kwa lipi? .
Gwajima ni Muongo. 
Kitendo cha kuhubiri uongo na kudanganya kuwa una ushahidi lakini huutoi huo ushahidi ni uthibitisho tosha ule ulikuwa ni uongo tuu wa mchana kweupe.
Bahati yake Makonda sio tuu ni Msukuma ambapo Wasukuma hawana makuu na wana madharau sana, hivyo amemdharau, bali pia Makonda ni Mlokole hivyo amemshtakia kwa Mungu, akalia machozi madhabahuni na kusamehe. 
Kwa Nini Gwajima ni Muongo? .
Kiongozi yoyote kabla ya kuteuliwa na rais, hufanyiwa vetting hivyo vyombo vya serikali vinazo taarifa zote sahihi kumhusu Makonda. 
Sasa tangu kutolewa kwa uongo huu, ungekuwa na ukweli hata chembe, tungeshuhudia hatua zikichukuliwa dhidi ya udanganyifu huu. 
Kitendo cha mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa dhidi ya Makonda ni uthibitisho kuwa vetting ilifanyika vizuri, jina la Paul Christian Makonda ni jina lake halisi, Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Na vyeti vyake ni vyeti vyake halisi ambavyo viko kwenye mamlaka yake ya uteuzi, hivyo Paul Makonda hapaswi kumuonyesha mtu yoyote vyeti vyake ili tuu kujibu uongo wa Gwajima. 
Sisi Watanzania wote katika umoja wetu ndio tuliomchagua kwa kura nyingi, Dr. John Pombe Magufuli awe rais wetu, kama rais wetu amemwamini Makonda, who is Gwajima kutuletea uongo na kuuamini. 
Wewe ambaye unajiita ni Mtanzania mzalendo, unawezaje kumwamini Gwajima kuliko unavyo mwamini rais wako?!.
Nikikuuliza kati ya uongo wa Gwajima kuwa Paul Makonda ni Daudi Bashite na ukweli wa rais Magufuli kuwa Paul Makonda ni Paul Makonda ndio maana mpaka sasa ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ubamwamini nani? .
Shuhudia jinsi Watanzania walivyo watu wa ajabu, yaani wanamwamini Mchungaji Gwajima kuliko hata rais wao! .
Utafiti na Sampling ya Watanzania. 
Utafiti huu uko based on jf, kuwatumia wana jf kama cross section ya sampling ya Watanzania wote. Ukipandisha bandiko lolote kumtetea Makonda, posts za kukupinga ni nyingi kuliko posts za kukosoa. 
Huu ni uthibitisho kuwa sisi Watanzania we don't think, name hata kwenye chaguzi zetu huwa tunajichagulia tuu kufuata mkumbo. 
When can we start to think kabla hatujaendelea kudanganywa tena na tena na tena?!.
Paskali.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.