Header Ads

Adai Pombe Ndio Imemfanya Akawa Mnene

Image result for wolperstylish instagram
Kuna usemi unaosema kuwa ‘Wasanii ni kioo cha jamii’ ambapo wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha jamii inafuata maadili, leo April 3, 2017 nimeipata stori hii ya staa wa Bongo movies Jackline Wolper ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwaonya vijana juu ya unywaji pombe.

Wolper alikwenda mbali zaidi na kuwashauri vijana ambao hawatumii pombe wajiepushe nayo, Jackline Wolper anatueleza sababu za kuandika hivyo.

“Niliandika kuhusu pombe kwa sababu naamini pombe labda ndiyo inaweza kuwa ilinifanya nikawa mnene kutokana na mwanzo mimi nilikuwa sinywi pombe kabisa na nilikuwa sijui kitu kinaitwa pombe na hata mtu alikuwa akinywa, mimi namshangaa kabisa. Kwa hiyo ndiyo nikaandika vile pombe siyo nzuri kwa wasichana ambao ndiyo wanaanza kujifunza pombe na wana miili yao mizuri tu. Waache kunywa pombe.” – Jackline Wolper.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.