Header Ads

Jifunze Namna Unavyoweza Kugeuza Makosa Yako Na Kuwa Mafanikio...!!!


Makosa katika safari yoyote ya mafanikio  ni kitu ambacho hakikwepeki. Bila shaka wewe na mimi tumeshawahi kukosea katika maeneo kadhaa ya maisha yetu. Kukosea huko kulitufanya pengine tujute au kuumia kabisa na kujiona kama vile hatufai.
Je, kitu cha kujiuliza hivi ndivyo tulivyotakiwa kuyachukulia makosa haya na kujihukumu vya kutosha. Jibu rahisi hapa ni hapana. Hatukuwa na sababu ya kujihukumu sana kutokana na makosa yetu, zaidi ya kugeuza makosa hayo na kuwa ushindi.
Na ni kwa namna gani tunaweza kugeuza makosa yetu kuwa ushindi?
1. Jifunze kutokana na makosa hayo.
Ili uweze kuwa mshindi na kugeuza makosa yako kuwa ushindi, ni lazima kujifunza kutokana na makosa ambayo unayafanya. Kama hujifunzi, hakuna utachokuwa unafanya, zaidi utaendelea kukosea na kubaki hapo. Wanaojifunza na kuchukua hatua ndio wanaofanikiwa.
Kukosea kwako hakuna shida sana, shida inakuja pale unaposhindwa kujifunza. Ni muhimu kujifunza kutokana na makosa yako na kurekebisha pale ulipokosea. Kwa kadri utakavozidi kujifunza utajikuta makosa yako yanageuka kuwa ngazi ya kukufanikisha badala ya vizuizi.

2. Chukua jukumu la kuwajibika.
Hautaweza kwenda popote wala kupata mafanikio, ikiwa utakuwa ni mtu wa kulaumu wengine kwamba ndio waliosababisha ukakosea. Mtu wa kwanza kuwajibika kwa makosa uliyofanya ni wewe. Acha kulaumu wengine, utakuwa unapoteza wako bure. Wajibika kwanza wewe.
Unapochukua jukumu la kuwajibika elewa wewe ndiye kiongozi wa maisha yako, hivyo kama kuna makosa yamefanyika kwa sehemu una mchngo wa kusababisha makosa hayo kujitokeza. Badala ya kulaumu, tafuta nini kilichokufanya ukakosea, kirekebishe baada ya hapo endelea na safari yko.
3. Jifunze kutokana na uzoefu.
Linaweza likawa ni jambo linalokuuma sana, hasa pale unapokosea. Lakini nina uhakika pamoja na maumivu hayo kuna kitu ambacho unaweza ukajifunza hapo. Kujifunza huko, huo ndio uzoefu ninaotaka uuchukue hapo na kuugeuza kuwa ushindi pengine yanapotokea makosa kama hayo kwa baadae.
Acha kuishia kuumia na kulalamika na ukabaki hivyo, utakuwa hufanyi kitu. Utumie uzoefu kukusaidia kufika kwenye kilele cha mafanikio. Mara nyingi kwenye kipindi cha kukosea unaweza ukakiona ni cha mateso na maumivu. Lakini , kumbuka siku zote uzoefu ni mwalimu mzuri w mafanikio yako.
4. Badili tabia zako.
Inawezekana ukawa unashindwa na unaendelea kufanya makosa kwa sababu ya tabia ulizonazo. Ili uweze kutoka hapo na kuepuka makosa huna namna nyingine zaidi ya wewe kuweza kubadili tabia zako mara moja. Ukiweza kubadili tabia zako hizo zinazokurudisha nyuma, basi yapo makosa ambayo unayarudia kuyafanya utayaepuka moja kwa moja na kuwa mshindi.
Hivi ndivyo unavyoweza kugeuza kushindwa kwako na kuwa ushindi wa mafanikio. Acha kuhuzunika na kusononeka sana. Fanyia kazi mambo hayo yatakuwa msaada mkubwa kwako sana.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.