Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

“Kutokula nyama ya kuku kumenifanya niishi miaka mingi” – Violet Brown


Baada ya kifo cha aliyekuwa binadamu mzee zaidi duniani Emma Morano’s wa Italia akiwa na miaka 117, April 15, 2017, rekodi hiyo sasa inashikiliwa na raia wa Jamaica Violet Brown aliyezaliwa mwaka 1900 ambaye ametimiza miaka 117 March 10 mwaka huu.
Wakati Emma Morano’s akitoa sababu yake ya kuishi miaka mingi kuwa kula mayai mabichi na kutokua na mume, Violet Brown kwa upande wake alipoulizwa kuhusu kinachomsaidia kuishi miaka mingi duniani, alisema kutokula nyama ya kuku na Nguruwe ndiyo siri ya mafanikio yake kuishi miaka mingi.

Hii sio rekodi pekee inayoshikiliwa na familia ya Violet Brown ambapo mtoto wake wa kwanza anashika rekodi ya kuwa mtoto mzee zaidi akiwa na umri wa miaka 97 ambaye ana mzazi aliye hai. Bi Violet Brown alipongezwa na watu mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness akitumia account yake ya Twitter na kuandika: “Binadamu mzee zaidi duniani ni Mjamaica Violet Brown, ambaye alizaliwa March 10, 1900. Hongera Violet.”

No comments:

Powered by Blogger.