Header Ads

MAGUFULI Atoa Onyo Kali Watakaotishia Muungano..!!!

RAIS Dk. John Magufuli ameonya kuwa mtu yeyote atakayethubutu kutaka kuvunja Muungano atavunjika yeye.
Ametoa onyo hilo jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Dk. Magufuli amesema kwa kutambua kuwa Muungano ndio silaha, jembe na ushindi wetu, atahakikisha yeye (Magufuli) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein wanaulinda kwa gharama yeyote.
Amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani na kuitunza ili muungano nao uweze kudumu milele. Mbali na Dk. Magufuli na Dk. Shein, viongozi wengine wandamizi waliohudhuria sherehe hizo ni marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete.
Wengine ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Makamu wa Rais Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.