Header Ads

Milioni 20 Zamtoka Shilole Eti Kisa Mgahawa Wake Tu...!!!

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, amesema kwa sasa amewekeza kiasi cha Sh milioni 20 kwenye mgahawa wake.
Shilole amesema kwamba, anashukuru Mungu kuona biashara yake hiyo inakuwa kila kukicha na kutoa ajira kwa vijana wenzake.
Alisema awali alianza na mtaji wa Sh 150,000 lakini amekomaa na katika usimamizi mzuri wa kibiashara sasa amewekeza kiasi hicho cha fedha.
“Nashukuru sana wateja wangu wanazidi kunisapoti kwenye kazi yangu, kwa sasa mgahawa wangu umeendelea kukuwa na tayari nimewekeza zaidi ya milioni 20 na pia nimeweza kuwaajiri vijana wenzangu ambao kwa sasa wapo 11,” alisema Shilole.
Pia Shilole amewashauri wanawake wenzake kutokata tamaa katika kazi zao kwani anaamini hata kidogo walichonacho kinaweza kuwafikisha kwenye malengo yao.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.