Header Ads

Prezzo Amnyoosha Shabiki Aliyemdhihaki Kuwa Anaringishia Gari la Mama yake


Rapper controversial wa hapa nchini Kenya, amezua msisimuko wa hisia kwa wapenzi wa mtandao wa Instagram baada ya kumjibu vibaya shabiki aliyeandika jibu la kumkejeli kwenye post yake ya Instagram.

Prezzo ni rapper ambaye wengi wanamuogopa kwa vituko vyake ambavyo haviishi, si nyuma ya pazia la camera bali hadi akiwa live on air kwenye runinga inayotazamwa na mamilioni ya mashabiki.

Katika muktadha huu, rapper huyo na staa wa reality TV show ya Nairobi Diaries alionekana kukerwa na jibu la Kelvin Masakhwi ambaye alimchana Prezzo kwa kuonyesha gari ambalo Prezzo anadai kuwa yake ya kwanza aliyonunuliwa na mamake mzazi alipokuwa chuo kikuu. Nikinukuu maandishi hayo, Prezzo amesema, “Old money fam, my 1st ride in uni had my lecturers looking at me in some type of way…. & u wonder why I love my mum to death. Gods son #Rapcellency.”

Tazama majibizano ya Prezzo na shabiki huyo kwenye picha hii hapa.Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.