Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

SHILOLE Unayoyafanya Instagram Mwanao Ajifunze nini...!!!?

 ZUWENA Mohammed, ni jina la binti mmoja mwenye simulizi ya kusisimua, akidai kubakwa akiwa kinda na kupewa mimba, ambayo kwa hali ngumu, alimudu kuishi nayo kwa miezi tisa na akajifungua mtoto mzuri  wa kike.
Lakini Shishi Baby au Shilole, ni msanii mwenye jina kubwa katika muziki wa kizazi kipya na uigizaji.
Hawa siyo watu tofauti, isipokuwa ni mtu mmoja aliyeishi katika mazingira mawili tofautitofauti, kutoka yale ya manyanyaso na dhiki kubwa, hadi ya kula atakacho, kufanya anachojisikia na kumudu mbwembwe zote za watoto wa mjini. Ninamfahamu kidogo Shilole, maana Zuwena sikuwahi kukutana naye.
Ni mwanamke jasiri, asiye na aibu katika kuhitaji kile anachokitaka na anafahamu, ili apate kila anachokitaka, ni lazima apambane yeye kama yeye. Katika hili, anasimama pale juu miongoni mwa wanawake wapambanaji.
Ni mcheshi pia huyu mdada. Ni aina ya mwanamke ambaye ni vigumu kumaliza kikao naye pasipo kufurahi, kwa sababu ya swaga zake, anapenda watu wafurahi na ndiyo maana ukimfuatilia sana, ni mwingi wa vituko vya kuchekesha. Umewahi kusikia kiingereza chake? Anajua anaongea ‘broken’ lakini hajali, ili mradi wale wanaojifanya wanajua, wanaelewa alikuwa anataka kusema nini.
Na akiwa jukwaani, ni mwanamuziki hasa, kwa sababu anaimba vizuri na anawajibika vyema katika kucheza na mashabiki wake kiasi kwamba hivi sasa, ni miongoni mwa mabinti wanaoishi kwa jasho lake mwenyewe.
Tatizo moja kubwa ambalo ninaweza kulizungumzia linalomhusu, ni namna anavyoshindwa kuyaishi majina yake mawili mazuri. Usisahau, Zuwena alipobakwa, akapata mtoto ambaye leo analelewa na Shilole.
Siku chache zilizopita, Shilole katika ubora wake, aliachia ‘clip’ moja katika akaunti yake ya mtandao wa Instagram, ikimuonyesha akijipapasa papasa mwilini, akijifunuafunua kuonyesha sehemu ya maungo yake, kana kwamba ni mtu anayehamasisha hamu ya kufanya mapenzi.
Huenda ni swaga zake kama nilivyosema pale mwanzo, lakini unapokutana na mtu ambaye tayari ni mzazi na isitoshe ni mwenye jina kubwa katika jamii yake, baadhi ya mambo si mazuri kuyafanya hadharani.
Ninamtazama mtoto wake ambaye sasa amefi kia umri wa kuweza kuperuzi katika mitandao, au ana marafi ki ambao wameshaanza kupitia mitandao, wanapoona picha kama ile wanapata wazo gani la ghafla?
Pengine kwa sasa anaweza kuona ni jambo la kawaida na inawezekana kabisa anafanya hivyo mbele ya mtoto wake kwa vile kwake ni kama burudani, lakini madhara ya jambo kama hilo ni makubwa kwa siku za baadaye kwa mtoto
wake, ambaye bahati mbaya, naye atajikuta akiishi kwa kuiga kutoka kwa mama yake.
Atapenda kujua mtu mwenye kujishikashika vile anamaanisha nini, anayetazama mtu akifanya vile anapatwa na hisia gani na vitu kama hivyo. Shilole amezidiwa na ustaa, kiasi kwamba anajisahau.

No comments:

Powered by Blogger.