Header Ads

Tajiri Aliyeoa Wake Wawili Ndani ya Saa 48 Aandika Historia


Kwa Javan Bidogo, wale wanaosema “penzi haligawanyiki” ni kama wanaamini msemo uliopitwa na wakati.

Bidogo, mwenye umri wa miaka 42, ameweza kuligawanya penzi lake kwa wanawake wawili ambao aliwaoa ndani ya siku mbili na kwenda nao fungate nje ya nchi kabla ya kurejea nchini ambako sasa anaishi nao nyumba moja.

Ndoa ya zaidi ya mke mmoja si jambo la ajabu, lakini Javan Bidogo na wake zake wawili waliibua mijadala takriban wiki moja iliyopita baada ya picha zao za harusi kurushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akiwa amevalia koti la kitambaa cha velveti cha rangi ya damu ya mzee, upande wa kushoto kukiwa na wasichana watatu na kulia wengine watatu, wote wakiwa wamevalia gauni za rangi hiyo kuanzia kiunoni wakati sehemu ya juu ikiwa ya rangi ya maziwa. “Sikutaka kuwakosa wote kwa kuwa ninawapenda kwa dhati. (Ndio maana) Nikafanya uamuzi. Nilizungumza na Asha (34) akakubali na pia Elvas (21) naye akabariki hilo. Kwa kuwa walikuwa wachumba zangu wa muda mrefu, niliona ni sahihi na nina haki kisheria,” alisema. Hata wake zake, Elvas Kulengwa na Asha Juma wanaonekana si tu kukubaliana na suala hilo, bali kufurahia ndoa hiyo ya mitala, wakionekana wenye tabasamu katika picha zote za harusi na nyingine ambazo zinaonekana kuchukuliwa kabla ya harusi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.