Header Ads

BILA Unafiki; Makonda Sikutegemea Haya Ungeyafanya Wewe Ukiwa Live

 

Nirudie bila ya Unafiki kiukweli leo nilikerwa na kushindwa kuendelea Kutazama kipindi cha Tuongee Asubuhi mwanzo mwisho.
Nilipatwa na Hasira kupelekea kuzima Tv na kuingia mtaani kutokana na Kile nilicho kishuhudia machoni mwangu japo ni kutoka Luningani!!
Hivi ilikuwaje Makonda ukubari kwenda /Kualika Tv kukuhoji ikiwa haukuwa Tayari!!?
Makonda Hivi Unajiamini vipi kucheka hovyo Ukiwa live tena kwamadharau Wakati ukitambua Unayo hojiwa ni mambo makubwa na si Masihala kabisa!!
Makonda unatambua wewe unapelekea kutukanwa kwa Rais wetu kipenzi na mtetezi wetu
unapata nafasi ya walau kututoa kimasomaso lakini bado unaweka petrol kwenye moto ulio kolea kweli!!
Nilipo sikia na kuona matangazo kupewa nafasi ya kueleza mbivu na Mbichi kuhusu Tuhuma zote ulizo elekezwa kwako
Nilipata nguvu kujua Sasa Star Tv wana jaribu kufuata utaratibu murua kumhoji mtu kabla ya kumtuhumu na kumuadhibu
lakini kiukweli niheri ungeendelea kukaa kimya kabisa!
Yaliyo tokea leo Yamekurudisha Nya 40% kuliko ulivyo kuwa Hapo jana na kuendelea nyuma.
Makonda kumbuka,Katika hii Dunia Mazuri 100 hupotezwa na baya moja(1) pekee
Tunafahamu unamengi Mazuri lakini Jichunge sana na Baya moja litakalo haribu mema yote.
Nini kilinikera leo!
1. Makonda hakuheshimu Mwenyekiti wa Mjadala ule,
Kweli yeye ni Mkuu wa mkoa
lakini pale alikuwa akihojiwa kama Makonda binafsi na Mkuu wa mkoa kama Wadhfa wake kama Tuhuma zilivyo elekezwa kwake,
kitendo cha Kumdharau Muongoza mjadala ni Upuuzi na Haliwezi kukubalika.
2. Kuchagua lipi uulizwe na lipi usiulizwe!!
Unaulizwa swali unatoa maelezo Yasiyo Endana na swali husika
Yasiyo endana na Kile tulicho Ambiwa au kuelezwa hapo awali kama lengo kuu la mjadala huo,
Nacho kifahamu ilikuwa utaulizwa maswali yoote na utayatolea ufafanuzi kulingana na tuhuma zako.
3. Makonda unacheka kwa dharau,kwa kejeli wakati wafahamu mahojiano hayo yapo live
kuna maelfu ya Watanzania wakitaka kujua je unaonewa au la!
4. Ulishindwa kujizuia na kutambua kuwa pale upo kama Makonda 90% sio kama Mkuu wa mkoa
mahojiano yale yalikuwa kujibu tuhuma kwa 80% sio kuelezea Nini kinaendelea mkoani kwako
kiasi kwamba Unakuwa mkali mpaka kuita watu Wanafiki!!
Kama hukuhitaji Mahojiano yale kwanini ukubari kuhojiwa!!?
5.Tunajua Aliye kuteua ni Kikwete
Ulipewa tuhumu ya kumpiga Warioba
lakini Jk aliona sio kweli na hata kama kweli ulikuwa sahihi hilo silihoji
ila Jk Akakuteua Kuwa mjumbe wa bunge la Katiba,
Haikutosha Jk akakuteua kuwa mkuu wa Wilaya,
Rais wetu akakuteua kuwa mkuu wa mkoa,
Hili halikufanyi Uchague swali lipi uuluzwe na mengine watu waende Kwa mamlaka zilizo Kuteua.
6. Unaonyeshwa picha ya Jumba na Gari
unakubari Vyako
lakini hutoi maelezo yeyote umevipataje!!
Kwa umli wako huo wa utumishi!!
Zaidi unakimbilia kutoa Kejeli,Dharau Kujiona!!
Bila kumung'unya maneno
Leo Makonda umenikera sana sana
nibora Ungegoma tu kuliko upuuzi huu ulio ufanya.
Star tv hawana lawama yeyote
wamefanya kile kinacho takiwa kufanywa,
Tuwape hongera kwa hilo.
NB
Haya ni maoni yangu binafsi
Tuache unafiki leo Jamaa Katia Doa Mahojiano yale
Credit Jamii Forum

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.