Header Ads

KIMENUKAA..Lema Amchana Live Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa Kumnyima Nafasi ya Kutoa Salamu za Pole Katika Msiba wa Wanafunzi Leo..!!


Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Godbless Lema ametoa masikitiko yake na kuonyesha kuumizwa na kitendo alichofanyiwa leo wakati wa kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva waliofariki katika ajali ya basi.
Lema anasema kitendo cha yeye kama Mbunge wa Arusha mjini pamoja na Meya wa jiji kunyimwa nafasi japo ya kutoa pole kwa familia na wafiwa wakati wa kuaga miili hiyo ni ubaguzi mkubwa. 
"Ninamshukuru Makamu wa Rais kuja kutoa pole kwa watu wa Arusha. Leo ni ubaguzi mwingine katika Taifa Mbunge na Meya kwa kunyimwa nafasi ya kutoa pole" alisema Goodbless Lema 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.