Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

LEMUTUZ Amchana Live Mchungaji Msigwa Kwa Kuingiza Siasa Kwenye Msiba wa Watoto Arusha

By @lemutuz_nation
Mchungaji Msigwa, ustaarabu ni kuwafariji wafiwa kwanza na kusubiri kuwazika marehemu yaani Wanafunzi watoto wadogo 32 waliofariki jana ...halafu ndio huko Chadema muanze kuingiza siasa zenu kuhusu Msiba ..ila kwa sasa wakati kuna Mama aliyepoteza Mume hivi karibuni na jana akapoteza Watoto 3 kwenye hii Ajali ya Taifa kwako wewe Mchungaji wa Kiroho kuandika maneno ya Kejeli kwa Rais na wafiwa ni UKOSEFU WA UTU NA HESHIMA KWA MAREHEMU NA WAFIWA ....Rais hata akimuandikia Mungu at this point and time haiwezi kuwarudisha Marehemu kuwa hai au kuwamalizia uchungu wafiwa ...kutafuta sifa za kisiasa kwa kutumia miili ya marehemu watoto wadogo Malaika wa Mungu ni Dhambi kwa Mchungaji kama wewe ....tunawasoma na kuwashangaa sana baadhi yenu huko Chadema kwa kauli za ajabu ajabu wakati huu wa msiba mzito kwa Taifa ...HEBU MUOGOPENI MUNGU KIDOGO .....KWENYE MSIBA MZITO KAMA HUU SIASA ZINATAKIWA KUFIKA MWISHO...tunatakiwa kunawaombea kwa Mungu awape wepesi wafiwa wote na Taifa zima katika kipindi hiki kigumu sana cha kukubali msiba huu mzito sana kwa Taifa ....hakuna mbaye hatakufa ila sidhani kama wewe ungependa ukifa mwanasiasa atumie kifo chako kutafuta sifa......again tunaomba Mungu afanye wepesi ili kesho Makamu wa Rais Mama Samia aongoze vyema mazishi ya Watoto wetu 32 waliopoteza maisha yao kwenye ajali mbaya Arusha jana ....MUNGU IBARIKI TANZANIA! - le Mutuz...

No comments:

Powered by Blogger.