Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Lulu Diva afunguka kushea Penzi na Shangazi Yake!


Ubuyu wa kutisha! Jipu limepasuka mjini kuwa muuza nyago na msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amekiri kushirikiana ‘kushea’ penzi la bwana mmoja na shangazi yake pamoja na shosti yake wa karibu.

Kwa mujibu wa Lulu Diva, jambo hilo limekuwa likimtesa moyoni lakini kwa kuwa anataka kuwa huru, basi ameona ni vyema akalipasua.

MSIKIE LULU DIVA

“Kila mtu anapitia mambo mengi sana kwenye uhusiano wa mapenzi na maisha kwa jumla. Nimeamua kufunguka kuhusu jipu nililonalo moyoni mwangu. Ni kuhusu jamaa mmoja ambaye nilikuwa ninampenda sana katika maisha yangu.UKIMSEMA VIBAYA…

“Kwa jinsi nilivyokuwa ninampenda yule jamaa, yaani ulikuwa ukiniambia kitu kibaya kuhusu yeye, basi ujue ni lazima nitaenda kumwambia na kukutaja. Nilikuwa sisikii wala siambiliki kwake.

AENDA KUMTAMBULISHA

“Kutokana na kudumu kwenye mapenzi kwa muda mrefu na kumuelewa, nilimuomba aje home (nyumbani) ajitambulishe ili tuwe huru, akafanya hivyo.

KUMBE ALISHA-DATE NA SHANGAZI

“Nilishangaa nilipomfi kisha pale nyumbani, watu wote wanamfahamu kama bwana’ke shangazi yangu. “Nilichoka sana kusikia vile, yule shangazi yangu, umri ni kama wangu kwa sababu tunatofautiana kama miaka minne au sita.NDUGU WAMKATALIA

“Kutokana na hali hiyo, ndugu walikataa katakata mimi kuwa na uhusiano na mwanaume huyo kwa sababu ya kuwa na uhusiano na shangazi yangu. Familia yangu ilikataa kabisa nisiwe na uhusiano naye.

AZIBA MASIKIO

“Kiukweli nilikuwa ninampenda sana yule jamaa, niliumia, lakini nikaziba masikio na kuwaambia kuwa mimi ninampenda na siwezi kuishi bila yeye.

AVISHWA PETE

“Basi nilivyowachomolea kuachana naye, jamaa alinivisha pete ya uchumba na tukaendeleza penzi letu.

ACHEZEA KICHAPO

“Pamoja na upendo niliokuwa nao kwa jamaa, lakini bado alikuwa akinidunda sana, nilikuwa nalia, nilivumilia kwa kuhisi labda ni sehemu ya mapenzi, lakini jamaa alikuwa ananipa kichapo.

AMFUMANIA NA SHOSTI WAKE

“Nahisi jamaa alikuwa kicheche sana kwani siku moja nilimkuta anazini na rafi ki yangu, tena kwenye kitanda changu. Niliumia kwani yule rafi ki yangu alikuwa ni kila kitu kwangu, nilimuamini na kumpenda kwa dhati.

JAMAA AFUNGWA

“Baadaye yule jamaa alipata matatizo akafungwa nchini Israel, tangu kipindi hicho sijawahi kuonana wala kuwasiliana naye.

MIAKA 2 BILA KUCHEPUKA

“Kutokana na maumivu yale na misukosuko ya mapenzi, niliamua kukaa kwanza bila kujiingiza kwenye uhusiano hadi miaka miwili ilipofi ka.

HANA RAFIKI WA KIKE

“Kutokana na kile kilichotokea nikawa sina imani tena na marafi ki kwani wao wanaweza kukuharibia maisha yako, ndiyo maana mimi sina rafi ki kihivyo,” alifunguka Lulu. Lulu ambaye kwa sasa amegeukia kwenye Bongo Fleva, anatamba na Wimbo wa Malele na Usimwache.

KUTOKA KWA MHARIRI

Yapo mambo mengi mabaya na mazuri ambayo yanafanywa na watu wengi kila siku, ingawa kuna mengine yanatesa kubaki moyoni hadi pale mtu anapoamua kuyatoa na kuwa huru kama alivyofanya Lulu.

No comments:

Powered by Blogger.