Header Ads

MSANII WA KIZAZI KIPYA MADEE ANASWA AKIWA AMEBEBELEA POCHI LA DEMU WA DJ
Msanii Madee (kulia) akiwa amebeba pochi la Snura jijini Tanga.
Wakiongea jambo.
Madee akipiga shoo ndani ya jiji la Tanga hivi karibuni.

Mwanamuziki Snura Mushi akifanya yake stejini.
Wacheza shoo wa Snura wakifanya yao stejini.
KATIKA hali isiyozoeleka, hivi karibuni msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Madee Ally, amebambwa jijini Tanga akiwa amebeba pochi la msanii wa kike, Snura Mushi, anayetamba na wimbo wake mpya wa Nionee Wivu aliowashirikisha Yamoto Band.
Snura alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alijibu kwamba kutokana na kushirikiana kupiga shoo katika jiji hilo, Madee alimsaidia kubeba pochi lake.
“Hili ni jambo la kawaida kwa wasanii kusaidiana na Madee ni kaka yangu, namheshimu sana na sina tatizo naye,” alisema Snura.
Madee alipotafutwa kujibu “mashtaka” hayo hakupatikana kupitia simu yake.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.