Header Ads

Mwanza:Inasikitisha sana Aliyemuua Mkewe kwa Risasi Kisha na Yeye Kujiua, Wote Wazikwa


MWANZA: ULE msiba mzito uliotikisa Jiji la Mwanza kufuatia mume kumuua kwa kumpiga risasi mkewe, kisha na yeye kujiua, miili ya wanandani hao imezikwa leo katika makaburi ya Kanyerere Mahina jijini humo.

Mtoto wa marehemu, Ester Maximilian akilia kwa uchungu kuondokewa na wazazi wake wote wawili.
Maximilian Ngedele Tulya (41) alimshambulia kwa kupiga risasi mkewe Thedy Patrickhadi kusababisha umauti wake usiku wa kuamkia Mei 26, 2017 ambapo ,u,e huyo naye alijiua kwa risasi.


Global TV Online ilikuwepo katika makaburi ya Kanyerere, Mahina Kata ya Butimba ambapo kulishuhudiwa umati mkubwa wa watu waliojitokeza kwenye mazishi hayo.

Waombolezaji wakiaga

Miili ya marehemu ikitolewa nyumbani
Shughuli ya mazishi ilianza na ibaada maalum ya kuaga miili ya marehemu ambayo ilifanyika nyumbani kwa marehemu hao, Kanyerere, Mahina kabla ya kupelekwa makaburini kwa mazishi.
Waombolezaji wakielekea makaburini kwa ajili ya mazishi.

Mtoto wa marehemu akilia kwa uchungu.
Mtoto wa marehemu, Ester Maximilian alionekana kujikaza na kusoma historia fupi ya maisha ya mama yake huku akibugujikwa na machozi hali iliyotia huzuni kwa waombolezaji waliofika msibani hapoGet it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.