Header Ads

NAPE Azidi Kuichachafya Serikali Bungeni..Adai Mikoa ya Kusini Hawataikubali Kamwe Serikali ya CCM ..!!!

Mbunge Nape Nnauye ljana bungeni wakati akichangia katika  bajeti ya Wizara wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji amesema Wanakusini hawatakubali kuona ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi unakwama kutokana na vita iliyopo kati ya mataifa makubwa.
Nape Nnauye amemtaka Waziri Mwijage asikubali kuona vita ya mataifa hayo inaendelea kuwaumiza wananchi wa Kusini na kusema kama atafanya hivyo  wao hawatakubali hilo jambo.
"Mwijage viwanda ni ukombozi hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa sababu bado ni masikini sana na ukombozi wowote una vita, hasa kwa wale ambao wanafaidika na mfumo wa kutokuwepo kwa viwanda. Na hapa nitatoa mfano. Tumekuwa tukizungumza juu ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi, Kilwa pale ila taarifa tulizonazo mataifa makubwa yenye 'interest' na mbolea katika nchi hii yanapambana kuhakikisha kiwanda hicho hakijengwi. Katika jambo ambalo hatutakubaliana nalo Mwijage ni pamoja na hili, kuruhusu vita hii iendelee kutuumiza wanakusini" alisema Nape Nnauye 
Nape Nnauye aliendelea kusisitiza
"Mataifa hayo yanapigana kwa maslahi yao na kama serikali mtayumba kwenye hili basi Wanakusini hatutokubali, tulishalizungumza, mlishakubaliana, mwekezaji alishapatikana na utaratibu uko wazi, sasa vita hii ya wakubwa isituumize sisi wakapiganie nje ya Lindi lakini tunakitaka kiwanda cha mbolea Lindi" alikazia Nape Nnauye 


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.