Header Ads

Nimekuta Chupi ya Mke Wangu Chumbani Kwa Mdogo Wangu wa Kiume

Jamani Leo ni Siku ya saba tangia nikute chupi ya mke wangu chumbani kwa mdogo wangu wa kiume,nimekaa nalo moyoni naona niwashikirikishe wenzangu nione mnishauri nini
Ni hivi Ninaishi na mke wangu,mwaka wa NNE sasa,tuna mtoto mmoja,nina Mdogo wangu,anaishi hapa tangia January niliponunua bajaj ili awe anaendesha ili kusaidia wazazi wetu nyumbani kijijini,sasa jumapili iliyopita Wife aliwahi sana asubuhi kwenda kanisani pamoja na mtoto, Mimi nilibaki nimejilaza mpaka kama SAA moja na nusu Hivi, nilivyokumbuka kuwa nilikuwa na Ahadi Fulani, katika kufanya maandalizi sikiweza kuiona pass, so nikaenda straight chumbani kwa dogo katika kuitafuta ndo nilipo kutana na chupi ya mke wangu, ambayo Mimi mwenyewe nilimununulia so imechoka choka kiasi chake,nilishikwa na butwaa kwani namwamini sana wife, dogo mwenyewe heshima kwa sana, nilichukua simu na kupiga picha kadha na kuzificha kwenye private vault, ile chupi nikaaicha palepale, wife hajasema chochote mpaka sasa, nawaza namna ya kuanza kumuulizia japo ameshahisi kuwa siko normal,coz nikimuona usoni nakuata hasira imepnada sana,kwa kifupi naogopa ukweli kuwa mke wangu amenisaliti kwa mdogo wangu,mpaka sasa simuoni kama mke wangu tena, namuona kama bundi kajificha chumbani kwangu, naomba mnishauri kwani Mimi kwa haraka haraka naona nimwite kaka yake aje amchukue kabla sijamfanya kitu mbaya, tatizo hasira zangu hupanda pole pole sana, kuzishusha ni kazi sana

By Shonkoso

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.