Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

SHILOLE - Harusi Yangu Utafungwa Kwenye Helkopta ..Sherehe Itafanyika Uwanja wa Taifa..!!!!


Shilole amesema lengo lake sio tuu kuweka rekodi au kuonyesha ana uwezo mkubwa kifedha la hashaa!! Lengo lake ni kutaka kila shabiki yake kuhudhuria kwenye tukio hilo la kihistoria ambalo litafanyika angani kabla ya helkopita kutua uwanja wa mpira wa Taifa ambako mashabiki wake watakutana kushuhudia harusi hiyo.
“Ndoa yangu nitafungia juu ya Ndege (Helkopita),Tukishuka nashukia uwanja wa taifa…,hivi unategemea mimi nitaolewa tuu halafu watu waone picha zangu tuu? Mimi nataka watu waje kushuhudia.Ujue mimi nina mashabiki wengi na wote nataka waje waone Dada Mwajuma aking’olewa“Alisema Shilole kwenye mahojiano yake na Clouds Fm.
Shilole ambae hakutaka kuweka wazi jina la mchumba wake huyo mpya ambae watafunga nae ndoa kwa kuhofia kuporwa na walimwengu alisema mipango ya ndoa ipo ingawaje bado kwanza kuna vitu havijakaa sawa na ikifika muda atawatangazia mashabiki wake.

No comments:

Powered by Blogger.