Header Ads

UBUYU wa Motomoto...Huyu Ndiye Waziri wa Magufuli Anaye Banjuka na Msanii Batuli..!!!

UBUYU ulionyooka kabisa umetua kwenye meza ya gazeti hili ukidai kuwa, waziri kijana katika serikali ya Rais Dk.John Magufuli ‘JPM’, amedata kinomanoma na penzi la msanii wa filamu Bongo mwenye shepu bomba, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Ijumaa lina full stori.
Awali zilivuja taarifa kuwa, waziri huyo wa wizara nyeti ambaye ni mume wa mtu (jina lake linahifadhiwa kwa sasa) kafa, kaoza kwa mrembo huyo ambaye ni kada wa CCM na hivyo ameamua kumng’arishia maisha yake ili aweze kumfaidi vizuri.
KISIKIE CHANZO
“Kama ni kuyapatia maisha, Batuli sasa hivi kayapitia maana mheshimiwa….(anamtaja jina) ndiyo kajiweka kwake sasa hivi, anamhudumia kwa kila kitu, ndiyo maana unamuona mambo yake sasa hivi supa kuliko hata mastaa wengine,” alimwaga ubuyu mtoa habari huyo kisha akaongeza: “Kampangishia mjengo kule Kunduchi na ndinga pia kamnunulia, nyie fuatilieni mtajua ukweli wa ubuyu huu ninaowapa.”
IJUMAA KAZINI
Baada siri hiyo kuvuja, mmoja wa waandishi wetu alimpigia simu Batuli na kumuuliza juu ya madai hayo ambapo alifunguka kuwa na uhusiano na mheshimiwa huyo ila akasema, hayo si mambo ya kuandikwa gazetini kwani ni maisha yake binafsi li kujiridhisha na habari hiyo, siku nyingine mwandishi mwingine alimpigia simu na kutaka kuonana naye kwa ajili ya mahojiano maalum ambapo, siku hiyo alimtaka paparazi huyo wakutane Bahari Beach, eneo la Bakery, Kunduchi jijini Dar.
Mwandishi alipofika eneo hilo, aliona gari la kifahari, Range Rover Discovery lenye rangi nyekundu na kulifuata, ambapo Batuli alimfungulia mlango na kuondoka eneo hilo huku wakiendelea na mazungumzo.
Licha ya kuzungumza mambo mengi siku hiyo, huku mwandishi wetu wakati mwingine akimrekodi, staa huyo alimtaja mheshimiwa huyo kuonesha kuwa ndiye
anayemuweka mjini.
SIKU ILIYOFUATA
Siku iliyofuata, mwandishi wetu alipotaka kuandika habari hii alisikiliza rekodi katika maelezo ya Batuli na akaamua kumpigia simu tena ili kujiridhisha pale alipomtaja mheshimiwa huyo kuwa ndiye anayemuweka mjini ambapo hakutaka kulizungumzia tena. Hata hivyo, mwandishi wetu alimtumia ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka hivi; “Batuli, wakati tunazungumza kabla ya ishu nzima, ulitamka mtu uliyenaye ni (jina la waziri)…” Batuli alivyojibu “Hilo siyo geni hapo kwenu (Global) kwa msaada muulize (akimtaja mmoja wa waandishi wetu aliyewahi kuongea naye)…”
IJUMAA KWENYE MJENGO ANAOISHI BATULI
Katika kuendelea kuchimba, hivi karibuni mapaparazi wetu walifika kwenye nyumba anayoishi Batuli iliyopo Kunduchi (Uzunguni) lakini baada ya kugonga geti alitokea mlinzi na kueleza kuwa, ni kweli staa huyo anaishi hapo ila hawezi kupatikana hadi mtu anayemhitaji awe na miadi (appointment) naye.
IJUMAA LAMSAKA WAZIRI
Katika kubalansi habari hii, waandishi wetu walitumia kila njia kumpata mheshimiwa huyo lakini hakuweza kupatikana hivyo linaendelea kumsaka ikiwa ni pamoja na kuhakikisha linamnasa akiingia kwenye mjengo anaoishi Batuli kisha tutawamwagia kila kitu hapahapa.
From GlobalPublisher


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.