Header Ads

ZITTO Aendelea Kupalilia Sakata la Serikali Kununua Ndege Mbovu....Adai Tumepigwa

MOROGORO WA NDEGE ILIYONUNULIWA AINA YA BOEING 787-8

Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha baada ya taarifa kutoka serikali kuwa imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.

Na ya kwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.
Kumekuwa na taarifa mbalimbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi.

Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbalimbali kutafuta ukweli.

Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi (Zitto Kabwe) nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.

1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508

-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea.

2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege z a mwanzo kutengenezwa zp

a Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwa hiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi.
Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa.

Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au Km 1609.344
Kutokana na hili makampuni yaliyotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea.
Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa.

Kutokana na aibu iliyokuwa indicate Kampuni ya Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo:-

(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege,

(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi (karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M).

CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tuliyo iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.

Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliyoagiza ndiyo moja ya zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens.

Swali lingine la kujiuliza kwa nini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M?

Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.

Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.

My take:
Iwapo humu tuna wataalamu wa ndege tupeni maoni yenu ili tupanue uelewa juu ya ndege hizi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.