Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Ben Pol Avunja Ukimya Kwa Ebitoke,Inasemekana wamekwichi kwichi kimya kimya

Ben amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya mchekeshaji Ebitoke kuonesha hisia za mapenzi katika mitandao ya kijamii kwa takribani majuma mawili hivi sasa.

"Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la kujifunza, ikiwa unampenda mtu au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la ikiwa haujaiomba kwa muhusika ?. Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale wawapendao.Pamoja na hayo, Ben aliendelea kusema "Ikumbukwe humu duniani sisi sote tunapita na labda huyo mtu kesho hatokuwepo. Ebitoke umenifundisha jambo kubwa sana maishani, najua wengi walikubeza sana wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na mimi laini huwezi amini mimi nimefurahi mno, kukutana na wewe na kuongea" alisisiza Ben Pol

Kwa upande mwingine Ben amesema amepata jambo kubwa sana kupitia Ebitoke na kuahidi kuyaishi maneno yake siku zote mwa maisha yake

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.