Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Du hii hatari sana jamani Gigy, Amber Lulu wamlipua Msanii Mwenzao Baby MadahaGigy Money
DAR ES SALAAM: Kufuatia kauli ya Mbon­go Fleva, Baby Joseph Madaha maarufu kama Baby Madaha, aliyoitoa hivi karibuni kwamba ma-video queen wanaojaribu kuimba ndiyo wanaharibu heshima ya Muz­iki wa Kizazi Kipya, baadhi yao wameibuka na kumlipua vilivyo mwanadada huyo.
Bila kuwataja majina, Baby Madaha alisema kwamba wauza sura kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, ambao wanaingia kwenye muz­iki kwa mgongo huo, wanaharibu
 muziki ambao wao wameujenga kwa muda mrefu.
Baby Madaha

“Ma-video queen wanaoingia kwenye muziki ilimradi tu, ndiyo wanaotuharibia huu muziki ambao tumehangaika na kuhaso nao kwa muda mrefu, kwa sababu wao wanaingia tu kirahisi ili­mradi wanajifunza jinsi ya kuimba basi bila ku­jua kwamba kuna watu tumepata nao shida,” alisema Baby Ma­daha.
Kutokana na kauli hiyo warembo ambao wanafanya u-video queen huku wakiwa ni wanamuziki pia wamemjia juu Baby
 Madaha na kumtolea maneno makali huku wakimtaka awe na heshima.
Warembo waliok­erwa na kauli hiyo ni Amber Lulu, Lulu Diva na Gigy Mon­ey ambapo mapo­vu yao waliyatoa kama ifuatavyo;
Amber Lulu
AMBER LULU
“Huyo Baby M a ­daha ni msham­ba, ame­shachoka hana kitu kipya kwenye muziki, siyo mbunifu kwa hiyo wivu wa kuona vipaji vipya na wasichana wazuri kama sisi Amber Lulu, Gigy Money na Lulu Diva ambao tumepitia video queen. tulimkuta kwenye gemu na tumempita, Baby Madaha ni ‘very cheap’ kwa kweli.”
GIGY MONEY (PICHANI)
“Kwanza huyo Baby Madaha simfahamu vizuri na ningekuwa mimi ndiye yeye nimetokea BSS, ungekuta sasa hivi niko staa mkubwa Afrika lakini kwa kuwa hajiongezi ndiyo maana yupo hivyo alivyo, atuambie ana nyimbo gani inayovuma sana au amefanya kitu gani kwenye muziki ambacho tunakiharibu? Aache dharau maana hata yeye anadanga tu kwenye muziki.”
Lulu Diva

LULU DIVA
“Huo ni mtazamo wake, kwanza simfahamu Baby Ma­daha hivyo nashindwa kumzun­gumzia sana, ila angetuambia kitu gani cha maana alichokifan­ya kwenye tasnia ya muziki, vid­eo queen ni kazi kama nyingine ila watu wamekuwa wakiidharau tu.
“Nilifanya kazi hiyo kama daraja la kuniwezesha kufikia malengo ya kuwa mwanamuziki na nimefanikiwa kwa hilo, hivyo Baby Madaha anatakiwa kuan­galia upya muziki wake yaani ni wapi alipokosea ili aparekebishe na siyo kusingizia watu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.