Header Ads

INASIKITISHA SANA BINTI MDOGO SANA KUTOKA DODOMA ALIVYOSETEKA NA UGONJWA HATARI SANA

Image may contain: one or more peopleSISI TULIOWAZIMA TUSEME MUNGU AHSANTE, SOMA HII TAARIFA YA KUSIKITISHA YA BINT HUYU ALIYEKUWA MUATHIRIKA WA UKIMWI JINSI ALIVYOPOTEZA MAISHA BAADA YA....!
Mwanzo mwa mwezi huu nilipokea taarifa za kushtua na kusikitisha juu ya kifo cha bint huyu pichana ambaye ni mwenyeji wa Mkoa wa Dodoma Wilaya ya Mpwapwa kijiji cha Tambi.
Huyu bint historia ya maisha yake ilikuwa ni ngumu sana, lakini kwa ufupi alikua Jijini Dar miaka ya 2004 kwa kufanya kazi za ndani na 2010 aligundulika kama ameathirika na HIV nakumbuka niliwahi kumfanyia mahojiano kipindi hicho nikiwa mwandishi wa Gazeti la Sani.
Binti huyo alisema hakukumbuki nani aliyemwambukiza maradhi hayo kwa tayri alikuwa ameingia kwenye mahusiano na wanaume kadhaa Jijini Dar kipindi akiwa anafanya kazi za ndan.
Baada ya kujigundua kama tayari ameathirika alikuwa mtu mwenye kukata tamaa ya kuishi tena na kumbuka nilifanyakazi kubwa ya kumtia moyo kiasi kwamba akajiona kama yu mzima kabisa na alianza dozi mara moja.Image may contain: one or more people
Hata hivyo kutokana na mazingira ya mjini ikizingatia alikuwa anafanyakazi kwa watu ilifhika mahara aliamua kurudi kwao Jijini huko Tambi DODOMA.
Bahati nzuri alikuwa na namba yangu ya simu na hakuacha kunipa maendeleo ya afya yake hatua kwa hatua na pia hata kumrushia kiasi cha fedha kwa ajiri ya kununulia matunda nilifanya hivyo kwa jinsi nilivyokuwa najaliwa.
Hata hivyo kadri siku zilivyokuwa zinakwenda msichana huyo akiwa kijijini alianza kukata tamaa ya kuishi tena kutokana na watu kumnyooeshea vidole kutokana na kudhoofu kwa afya
yake.
Msichana huyu mrembo aliendelea kuteseka na mardhi hayo hatari duniani lakini pia kipindi hicho akiendelea kutumia dawa hizo za kurefusha maisha alikuwa amefanyiwa upasuaji zaidi ya mara mbili sehemu za shingoni kwa nyuma baada ya kuota uvimbe ambao ulielezwa ulisababishwa na dawa hizo ambazo kimsingi mgonjwa ukizitumia muda mrefu hutengeza sumu.
Hali hiyo ya maumivu ilipelekea msichana huyo mwanzoni mwa mwaka jana kugoma kuendelea kunywa dawa hizo kwa madai zimemchosha kutokana na wingi wa dawa hizo na msharti yake kuwa lazima uzinywe kila siku kwa muda ule ule bila kupitilia.
Lakini pia dada huyo aliona bora umauti umkute kuliko kuendelea kuteseka na ugonjwa huo unaotesa sana na kuabisha machoni mwa watu ambapo afya yake iliendelea kudhoofu sana lakini kutokana n alimu duni za watu wa vijijini kushindwa kumlinda na kumsimamia mtu wa namna hiyo familia yake waliamua kumuacha.
Hata hivyo msichana huyo alipofika hatu ambaya aliacha ujumbe mzito ukiwataka familia yake kulinda afya zao kwa maana maumivu aliyokuwa anayapata hakutaka mtu mwingine katika familia yake ayapate.
Lakini pia katika ujumbe huo aliwasihi sana watu kuacha zinaa maana ndiko gonjwa hilo linakopatikana kiurahisi, hatimae mwanzoni mwa mwezi huu wa sita mschana huyo alifariki akiwa na maumivu makali.
Kama wewe na mimi tuwazima hakika tuendelee kulinda faya zetu kwani ndiyo utajiri mkubwa kuliko fedha. Tusiwe na kiburi cha uzima tukasahau kuwa mardhi yapo hasa UKIMWI ambao unaua unatesa unaaibisha na kuumiza.
Ubarkiwe rafiki yangu
Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.