Header Ads

Jack Wolper Afunguka Ndoa yake na Ali Kiba

Staa wa filamu za Kibongo asiyepungukiwa mbwembwe kwenye mapenzi, Jacqueline Wolper.
 Stori: Ally Katalambula, Amani, Habari

UTAMU wa ubuyu ukae chini na umung’unye taratiiibu! Staa wa filamu za Kibongo asiyepungukiwa mbwembwe kwenye mapenzi, Jacqueline Wolper, amefunguka kuwa ilibaki kidogo tu aolewe na msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba kama wasingekuwa mastaa maishani mwao.

Gazeti la Amani  lilizungumza na Wolper ambaye alidai kuwa penzi alilolikuta na kulipata kwa Kiba ni penzi ambalo hawezi kulisahau maishani mwake.

ASIMULIA PENZI LA KIBA LILIVYO

“Ni mtu mwenye upendo wa kweli, anajua kujali, anathamini na ninaamini moyo wangu ulimpenda kwa dhati.

WALIVYOKUTANA

“Sikumbuki ilikuwa mwaka gani, ninachokumbuka ilikuwa ni Mtaa wa Lindi uliopo Kariakoo wala sikumbuki nilienda kufanya nini siku hiyo.

MUDA WALIO-DATE

“Ni muda mrefu, maana imekuwa siku nyingi. Kipindi hicho wote hatukuwa na majina makubwa (mastaa) kama tuliyonayo sasa. Tulipendana na tulikuwa na matarajio makubwa mbeleni.

KUTENGANA KWAO

“Baada ya kuwa mastaa, kila mmoja akajiona mkubwa zaidi ya mwenzake, ndoto na matarajio yote yakatoweka, polepole penzi likaanza kuyeyuka na hatimaye kufa kabisa, ingawa hatujakoseana kihivyo kiasi cha kushindwa kusalimiana kama wengineo. Naamini tulipendana lakini usupastaa ukazidi nguvu ya penzi letu.

ANACHOKIKUMBUKA KWA KIBA

“Mengi nakumbuka, kubwa ni upole wake pamoja na unyenyekevu, hii ni tofauti na wanaume wengine ambao nimewahi kukutana nao.

KUHUSU KURUDIANA NAYE

“Swali hilo naomba nisilijibu na ibaki kuwa siri yangu, ingawa ni muda mrefu na kila mtu ana mambo yake mengi zaidi,” anasema Wolper

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.