Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Kwa Wasanii Wenzake...List Aliyowakosea Adabu Hii Hapa


baraka The Prince
MOJA YA SIFA MUHIMU KATIKA MAFANIKIO NI NIDHAMU NA HASA KUHESHIMU WAKUBWA AMBAO WAMEKUTANGULIA.

Nadhani tunaweza muona msanii @barakahtheprince_ toka ameanza muziki tunakuwa tunamuona kama anaenda mbele kimataifa lakini mwisho wa siku anabaki hapa hapa.Sawa tuseme labda ngoma zake hazijawa na nguvu kwenda kimataifa ila nje ya hapo kuna maswala ya msingi ya kuangalia.

Nadhani moja ya kitu ambacho @barakahtheprince_ kitakuja kumfelisha ni kutowaheshimu wasanii wenzake ambao ni wakubwa kwake na hata wamemtangulia kwenye game.

@barakahtheprince_ ashawahi kuingia kwenye mzozo na @naytrueboy na kuongea mambo mabovu zaidi kwa ney lakini mwisho wa siku nay alikuja akaona huyu ni mtoto na akaepusha malumbano.

Lakini pia @barakahtheprince_ ashaingia kwenye mzozo na @msamibaby na alimtukana msami maneno mabovu lakini kumbe msami alichofanya alimtania tu kuhusu najma mwisho wa siku barakah akamtukana msami bila sababu.

Lakini ni @barakahtheprince_ huyu huyu leo anamuongelea maneno mabaya @iambenpol na kumuambia sijui katoa wimbo mbaya sijui kajidhalilisha.Kwa mtu kama barakah anatakiwa kumuheshimu benpaul mana kwanza ni kama kaka yake na pia kamtangulia kwenye game na bado uwezo wa benpaul ni mkubwa kuliko barakah na pia benpaul ni mtu mwenye nidhamu ambaye sikutegemea mtu kama barakah atamuongelea maneno hayo.

Ila ni huyu huyu @barakahtheprince_ ambaye alishindwa hata kumuheshimu msanii wa mkoa wake @youngkillermsodokii na kusema wazi hajawahi kuwa shabiki wake na wala hajawahi penda wimbo wake wowote ki hekima sio jambo zuri hasa ukizingatia anatoka naye mkoa mmoja.

Ila ni barakah huyu alimdhihaki @diamondplatinumz na kusema kuwa alijua simba ni mnyama mkali kumbe ni kamnyama kadogo tu kaoga akimlenga diamond sababu anajiita simba.

Haya yote ukiyaunganisha unagundu ndio msanii anaongoza kwa kutokuwa na nidhamu na wasanii wenzie

No comments:

Powered by Blogger.