Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Licha ya Mwezi Mtukufu… Lulu Diva Adaiwa Kuishi na ‘Serengeti Boy’


EXCLUSIVE! Ubuyu wa ‘town’ unaoenea kwa kasi ya kiberenge unamhusu msanii na muuza nyago kunako video za Kibongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ kudaiwa kuishi na kijana aliyemzidi umri ‘serengeti boy’ (jina kapuni) na kwamba ndiye anayemuweka mjini kwa sasa.
Kwa mujibu wa chanzo kinachoongozana na staa huyo mara nyingi, Lulu amekuwa akijitenga na marafiki zake kuficha aibu ambapo amekuwa akihudumiwa mambo mengi na serengeti boy wake.
“Sijui anafanya kazi gani lakini ndiye anayempa jeuri Lulu kwa sasa. Anamsimamia kila kitu kuanzia kwenye muziki hadi mjengo anaoishi,” kilibonyeza chanzo.
 Ili kubalansi mzani wetu, Star Mix lilimtafuta Lulu kujibu madai hayo kama yana ukweli na alipopatikana alifunguka;
“Nyie mmepata wapi hizo habari? Kwa taarifa yenu tu najihudumia mwenyewe na sijawahi kuishi wala kumilikiwa na serengeti boy sijui! Kama unabisha njoo kwangu….tii tiii tiiii tiiiiii…” akakata simu

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.