Header Ads

Mastaa Mwezi Huu Kanzu Kama Kawa, Ushungi Kwa Sana, Swaumu Zinapanda? Au mnatuzuga tu na mashungi yenu?

Idris Sultan
IKIWA imefika Ramadhani ya 14 Ijumaa ya leo, wapo mastaa ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa sambamba na Waislamu wote tangu kuanza kwa ibada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha mashabiki wao na watu wengine kufunga, kufuturisha na kusaidia wasiojiweza katika mwezi huu mahususi kwa mfungo.

Lulu Diva
Pia wapo mastaa ambao kwa kipindi hiki ‘wameamsha dude’ kupitia mitandao yao ya kijamii kwa kutupia picha wakiwa wamevaa mavazi ya heshima ambayo ni alama kwa dini ya Kiislamu.
Baadhi yao ni staa wa vichekesho, Idris Sultan wasanii wa Bongo Fleva, Shetta, Chegge, Snura na wengine wengi. Ukweli ni kwamba katika hili kwa namna moja ama nyingine mastaa wameonyesha kujitambua na kuelewa kuwa wao ni kioo cha jamii. Kwamba, ilihali wana wafuasi wengi kwenye mitandao yao ya kijamii bila shaka wapo watu wengi sana watahamasika kushiriki ibada ya Mfungo wa Ramadhani kama wao.
Lakini pia kusaidia watu na hata kutenda matendo mema katika mwezi huu mtukufu. Unaweza kuona hapo ni kwa namna gani baadhi ya watu watakavyofaidika kupitia wao kufunga na kushiriki ibada ya Mwezi Mtukufu ipasavyo ama watu wengine watakaoona wanayofanya na kujitolea kwa moyo kama mastaa hao.

Lakini pia kitendo cha baadhi ya mastaa kusitisha kazi zao akiwemo Idris Sultan ambaye amezungumza na Showbiz na kusema kuwa amesimama baadhi ya kazi za sanaa kwa sasa ili ashiriki ipasavyo mfungo ni jambo la kupongezwa.
Katika hali ya kawaida kila mmoja anatakiwa kufanya ibada kupitia dini anayoamini. Kuhamasishwa kufanya ibada ingawa ni wajibu kwa baadhi ya watu, si jambo jema na katika Showbiz ni jambo kubwa ambalo kwa namna moja ama nyingine mtu akiweka pongezi si mbaya. Showbiz inawapongeza mastaa wote wanaoshiriki mwezi wa mfungo na kujitolea kwa kila hali kile walichonacho kama fadhila kwa jamii inayowasapoti katika kazi zao.


Hata hivyo, kupitia ukurasa huu siyo mbaya tukashauriana mambo kadhaa ya kufanya katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Radhamani hasa kwa wale walio Waislamu na wasio.
Lakini kabla ya kushauri, niwaulize tu nyie ambao kila wakati mko ndani ya kanzu, hijabu na baraghashia, hivi swaumu zinapanda au mbwembwe tu? Kama zinapanda basi swadakta lakini kama ni mbwembwe, Mungu anawaona. Ya kufanya sasa! Ni kipindi cha kumfurahisha Mungu kwa kutenda mema na kuacha mabaya.
Najua si kwa kipindi hiki tu lakini ni vyema ukautumia mwezi huu kuongeza ibada na kumuomba Mungu akusaidie katika kazi zako zinazokuingizia kipato halali. Pia saidia wasiojiweza, futurisha walio na uhitaji na siyo kwa mbwembwe. Hiyo itakufanya uwe katika mazingira mazuri ya kumfurahisha Mungu wako

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.