Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Mastaa Wengi ni Wasumbufu Kwenye Mapenzi – Amber lulu


Video vixen na mwanamuziki kutoka hapa Bongo Amber Lulu amebainisha kuwa mastaa wengi katika kiwanda cha burudani ni wasumbufu sana ukiingia nao katika mahusiano ya kimapenzi.Amber mwenye Lulu zake amebainisha hayo kupitia Bongo Dot Home ya Time Fm kuwa ” Mastaa wengi bongo ni wasumbufu sana, mimi huko nyuma niliwahi kuwa katika mahusianio na hao mastaa nikaona aah basi bora niachane nao, naona walivyo kwa sasa na najua wanavyoishi ndio mana sina mpango nao.”

“Wastaa wengi hawako serious sana na hata kwenye maisha yao hawako serious, mie naona mastaa naoshindanao naona kabisa hata akiwa na mpenzi kuna kitu kinamiss , unakuta mtu anakaa na watu hata watano yani,” amesema Amber.

Kwa sasa mrembo huyo ameelekeza nguvu zake katika muziki na huwenda tusimuone mara kwa mara akitokea katika video za watu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.