Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

MSAMBWANDA WA BANDIA WA ANTI LULU WAYAYUKA KIULAINI BILA KUTUMIA NGUVU


DAR ES SALAAM: Mwanadada anayesifika kwa kutingisha wowowo lake hasa awapo kwenye kundi la watu, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ amepukutika ghafla na kalio au msambwanda wake kuyeyuka hivyo kuibua mshangao kwa watu wanaomfahamu.
Wikienda lilimnasa Anti Lulu wikiendi iliyopita na kumfotoa picha zinazomuonesha hana msambwanda huku akiwa amekongoroka ambapo alipobanwa kulikoni, alisema kuwa, amekonda kwa sababu amepata mpenzi wa Kizungu ambaye anataka awe na mwili mdogo.
“Nimepata mpenzi Mzungu, ameniambia nipungue ndiyo maana hata kalio langu limeisha, atakayenisema nina Ukimwi aje twende nikapime achukue majibu maana niko safi hivyo sina hata presha kwamba ninakonda kwa sababu gani, kukonda ukiwa unajua afya yako ni salama na kuna raha yake,” alisema Anti Lulu.
Anti Lulu aliwahi kukaririwa na gazeti hili akieleza kuwa, kutokana na kuwa na kalio kubwa amekuwa akisababisha ajali kwa wanaume ambao humshangaa na kwamba endapo litaondoka, itabidi aende kwa mchungaji ili akaombewe lirejee

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.