Header Ads

Professor Mkumbo Achafua Hali ya Hewa Kwa Kuamua Kuwatolea Uvivu Wapinzani Kwa Kuwaambia....

Prof Kitilya Mkumbo

Katika hali isiyo ya kawaida ambayo sidhani kama pia itavumiliwa na Wapinzani wa nchi hii ( hasa CHADEMA ) Mwanasiasa, Mchambuzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Professor Kitila Mkumbo ameamua kuwatolea uvivu Wapinzani wa nchi hii hasa hasa wa CHADEMA baada ya kuandika katika Kurasa yake ya Tweeter kwamba nanukuu

" Wapinzani wa nchi hii wanaugua Ugonjwa mpya uitwao Opposition Defiant Disorder ( ODD ) ambao huathiri mfumo wao mzima wa Kufikiri / Kuwaza na kuwapelekea Wapinzani ( CHADEMA ) kila mara na kila siku wao kuwa ni wapingaji tu wa kila kitu hata kama kina manufaa kwa nchi hii / taifa hili na kwamba Wapinzani ( hasa CHADEMA ) wanastahili haraka sana kupata Tiba ya akili ili waweze kutambua kuwa kuwa Mpinzani haimaanishi kupinga tu kila kitu " mwisho wa kumnukuu.

Je mnadhani huyu Professor na Msomi aliyetukuka kabisa Kitila Mkumbo kwa kauli yake hii yupo sahihi na pengine labda wahusika Wapinzani ( hasa hasa CHADEMA ) wanatakiwa kubadilika haraka na wakapate kweli Tiba ya Ugonjwa wao unaowasumbua wa ODD au labda Yeye Professor Kitila Mkumbo ndiyo amekengeuka / amepotoka na yawezekana Yeye ndiyo amewehuka / kawa wa hovyo hovyo hivyo anahitaji kutangulia kwenda Milembe Hospital Mkoani Dodoma kupata tiba.

Mjumbe hauwawi!

Nawasilisha.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.