Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Ukweli Mchungu..Wabunge Waliotumia Muda Wao Kuishangilia Bajeti Wajipime Sana, ni Kitendo cha Aibu Walichofanya..!!!

Hawa watu sijui tuwaelimisheje. Wanakutana eti na kipengele cha kuondoa road license kwenye bajeti wanapiga makofi na kushangilia kijinga kabisa. 
Wakikutana na kipengele kigumu kwao wanakaa kimya kwa muda ila kikija kizuri tu kwa sura tena hata ambacho hawakielewi wanaanza kushangiliashangilia hovyo hovyo tu. 
Pale badala wangetumia muda wao kusikiliza kwa makini tena umakini mkubwa, wachambue na kuandika mambo muhimu wanabaki kupiga mayowe tu! 
Baada ya kutoka weupe jana kwa kushangiliashangilia kitakachofuata ni kuchangia vitu visivyo na maana na bajeti inapita na mapungufu yake mengi tunarudi tena mwakani na ujinga ule ule wa kila siku. 
Spika naye anaingia kwenye mkumbo wa ushangiliaji huku akiwa na lengo la "kuwaondoa wabunge wake wa CCM kwenye umakini kama ambavyo wanafanya siku zote" Huu ni utapeli wa kisiasa. 
Inakera sana kuwaona hawa watu wakifanya mambo ya kitoto kabisa.
Chanzo JF


No comments:

Powered by Blogger.