Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

UNAAMBIWA ZARI THE BOSS LADY AVAA SURUALI NA KUTAKA KUZICHAPA NGUMI KWENYE KIKAKO CHA FAMILIA

Image result for zari the boss lady husband

KAMPALA: Watatoana roho Yarabi kwa mali alizoacha marehemu! Wengi walitabiri kuwa, kufuatia mtifuano mkali juu ya mali alizoziacha mumewe aliyefariki dunia Mei 25, mwaka huu, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’, aliyekuwa mkewe, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ipo siku atazichapa kavukavu na hasimu wake aliyekuwa msiri mkubwa wa baba watoto wake huyo, Lawrence Muyanja ‘King Lawrence’. Aliyekuwa mkewe marehemu Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. WATAKA KUVUNJANA SHINGO
Hicho ndicho kilichodaiwa kujiri hivi karibuni ambapo Zari na King Lawrence, ilibidi waamuliwe baada ya kutaka kuvunjana shingo kwenye kikao cha familia ya Ivan kilichofanyika nyumbani kwa marehemu, Muyenga jijini Kampala, Uganda. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kilichoutonya mtandao maarufu wa habari za udaku nchini humo, Zari na King Lawrence walitaka kutoana roho mbele ya ndugu wa karibu waliokuwa wamekutana kujadili jinsi mali zilizoachwa na marehemu Ivan zitakavyosimamiwa.
UAMUZI WA KUSHANGAZA
Ilidaiwa kuwa, kilichosababisha tafrani hiyo ni kufuatia familia ya Ivan kupitisha uamuzi wa kushangaza kwamba, mali hizo zisimamiwe na King Lawrence, jambo ambalo lilimfanya Zari acharuke kisha kuvaana na jamaa huyo kabla ya kuamuliwa na kikao kuvunjika kwa muda. Hata hivyo, ilielezwa kuwa, katikati ya kikao hicho, familia ilidai kutoa tamko hilo kama mapendekezo tu ili kufungua mjadala wa ishu hiyo kwa sababu King Lawrence alisemekana kujua orodha ya mali zote za Ivan, lakini Zari aligeuka mbogo na macho yake kubadilika rangi na kuwa mekundu

No comments:

Powered by Blogger.