Header Ads

Unakumbuka alichofanya Chris Brown Kenya? Damian Marley naye kakifanya

Mwimbaji staa wa Raggae kutoka Jamaica ambaye ni mtoto wa Legend katika miondoko hiy Hayati Bob Marley, Damian Marley ‘Jr. Gong’ yupo Africa kwa music tour ambapo moja kati ya nchi ambazo ameshafika na kufanya show ni Kenya na kuacha gumzo.
May 31, 2017 Damian Marley alifanya show Kenya lakini gumzo kubwa haikuwa show bali kitendo chake cha kudaiwa kumpotezea shabiki mwanamke ambaye alitaka kupiga naye selfie akiwa na mtoto mara tu baada ya staa huyo hutua Jommo Kenyata International Airport.
Kitendo hicho cha Damian kinataka kufanana na kile alichokifanya staa wa R&B kutoka Marekani Chris Brown alipofika Kenya kwa ajili ya Mombasa Rocks Festival ambapo alidaiwa kuvunja simu ya shabiki baada ya kutaka kupiga naye picha.

Ratiba ya ziara ya Damian Marley barani Africa
Kitendo hicho kilipekea Mwandishi mmoja wa Habari Kenya kulaani Damian kukataa kupiga picha na mwanamke kwenye video iliyosambaa ambayo pia alitoa maneno makali kwa staa huyo.
Video: Muhudumu wa Hoteli aliyevunjiwa simu na Chris Brown Mombasa >>Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.