Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

VIDEO: Sakata la Kusimamishwa Bungeni, Halima Mdee, Ester Bulaya Kumpeleka Ndugai Mahakamani


NA HILLARY DAUDI | GLOBAL TV ALIYEKO KILIMANJARO

IKIWA ni siku chache baada ya Spika Job Ndugai kuwasimamisha wasihudhurie Bunge hadi mwakani, mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Ester Bulaya wa Bunda Mjini wote wa Chadema wamefunguka ya moyoni na kumtolea uvivu spika huyo kwamba asidhani yupo juu ya sheria huku wakiahidi kutinga mahakamani kuidai haki yao.
Wakiwa mkoani Kilimanjaro kwenye mazishi ya mzee Philemon Ndesamburo, wabunge hao walipata fursa ya kuzungumza na Global TV Online kuhusiana na adhabu hiyo, na hiki ndicho walichokisema.
Kwa upande wa Ester Bulaya, alidai Ndugai amekuwa kiongozi wa uvunjifu wa amani bungeni akifuatiwa na wafuasi wengine wa CCM, lengo lao likiwa ni kuwanyamazisha wapinzani. Akakumbushia tukio la spika huyo kumpiga mpinzani wake wakati wa harakati za kura za maoni na kumuelezea kwamba ni mtu asiyewedha kudhibiti hasira na ambaye viatu vya ubunge havimtoshi.
Bulaya alisema yeye ndiye aliyewashawishi wenzake wagome na kutoka bungeni lakini alifanya hivyio kama kiongozi kuwalinda wabunge wake wasiendelee kutukanwa na kudhalilishwa na wafuasi wa CCM.
Kwa upande wa Halima Mdee, yeye alisema Ndugai na wabunge wa CCM lazima waelewe kwamba bunge linaongozwa kwa sheria na kwa sababu hii si mara ya kwanza wao kusimamishwa, watakwenda mahakamani kuhakikisha haki inapatikana.
Mdee aliongeza kuwa Ndugai anajua kwamba alifanya makosa ndiyo maana anaogopa wao wasiende mahakamani lakini lazima watafute haki mahakamani. Akazungumzia suala la polisi wa bunge kuondolewa bungeni kwa kushindwa kumshughulikia Mnyika kisawasawa kuwa ni dalili ya hatari kwa bunge


No comments:

Powered by Blogger.