Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

WEMA SEPETU ASOTESHWA MAHAKANI HUKU MFUNGO UKIMTETEMESHA MWILI MZIMA UTADHANI ANA DEGEDEGE


DAR ES SALAAM: Mrembo Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, juzi Alhamisi alijikuta akisota licha ya kuwa katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Wema ‘Madame’ alifika mahakamani hapo saa mbili asubuhi akiwa ameambatana na watu watatu kwenye gari aina ya Toyota Brevis, wawili kati yao wakiwa ni wasaidizi wake wa ndani, Matlida Abas na Angelina Msingwa ambao pia ni washitakiwa pamoja naye.
Baada ya kufika mahakamani hapo, Wema alisota kwa saa kadhaa akisubiri kesi yake kusomwa, ambapo hata baada ya muda wa kesi kufika, alipoingia kortini alisubiri kwa muda mrefu kabla ya shauri lake kuitwa, hali iliyomfanya aonekane kama aliyemaindi kwa kusoteshwa.
Mahakamani hapo ilidaiwa na upande wa mashtaka kuwa kwa nyakati tofauti Aprili 3 na 4, mwaka huu, Wema alionekana akinunua na kutumia dawa za kulevya (bangi) katika eneo lisilojulikana, lakini pia alikutwa na vipande vidogo vya msokoto wa kilevi hicho nyumbani kwake kufuatia ukaguzi uliofanywa na polisi.
Upande huo wa mashitaka ulieleza pia miongoni mwa ushahidi wa Wema kujihusisha na madawa ya kulevya unatokana na jina lake kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Hata hivyo, Wema alikana mashitaka yote na kesi hiyo kuahirishwa na kupangwa tena kusikilizwa Julai 14, mwaka huu.

No comments:

Powered by Blogger.