Header Ads

HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUWA, HATIMAYE SHILOLE ATOLEWA POSA NA HUYU HAPAZuwena Mohammed ‘Shilole’
UBUYU unaomung’unywa taratibu mjini unamgusa mwanamama aliyetokea kwenye filamu za Kibongo kisha akajikita katika Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ au ‘Shishi Baby’ ambaye taarifa rasmi zinasema kuwa ametolewa posa kimyakimya na hivi karibuni anatarajiwa kuingia kwenye ndoa.
ATAKA IWE SIRI KUOGOPA ‘TEAM FISI’
Kwa mujibu wa chanzo makini, juzikati Shishi alitolewa posa na mwanaume ambaye hakuwekwa wazi kwa kuwa staa huyo amekuwa akitaka kuifanya ishu hiyo kuwa siri.
“Si unawajua tena mastaa wetu? Hawachelewi kufanya yao ndiyo maana Shishi hataki kumwanika mwanaume wake kwa madai kwamba anaogopa wajanja wasije wakapita naye kama ilivyo kwa yule aliyekwapuliwa na Nisha (mwigizaji Salma Jabu).
“Baada ya mbilingembilinge nyingi za mjini, hatimaye Shishi sasa anaolewa na hapa tunapoongea ndiyo kwanza watu wamerudi Dar kutoka Igunga (Tabora) nyumbani kwa akina Shishi kupeleka posa.
“Kwanza ishu ilikuwa ni kumtambulisha mwanaume kwao ndipo wakaona wamalize kabisa na suala la posa hivyo kifuatacho ni kufunga ndoa ambayo nasikia itakuwa ndani ya mwaka huu,” alinyetisha mtoa ubuyu wetu kwa sharti la kutochorwa gazetini kwa madai kuwa anamjua vyema Shishi, hachelewi kumuanzishia mtiti.

Shishi Baby na Nuh Mziwanda.

SHISHI ABANWA, AFUNGUKA
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, kama ilivyo desturi yake, Ijumaa Wikienda lilimsaka Shishi ambaye mwanzo alitia ngumu lakini baada ya kubanwa vizuri, alikiri kuwepo kwa ishu hiyo.
Alipoulizwa mwanaume aliyemchumbia ni nani au ana wasifu gani, Shishi alifunguka:
“Wewe ujue tu ni kweli nimechumbiwa lakini kuhusu kumwanika mtarajiwa wangu, kwa kweli sipo tayari. Maana kwa upande wa wanaume wanaonyatia wanawake wa watu wanaitwa Team Fisi, sasa sijui kwa upande wa wanawake. Au tuseme Team Fisi kwa upande wa wanawake.
“Lakini kimsingi mchumba wangu ni mtu wa kawaida sana na siyo staa,” alisema Shishi na kutoa mwanya kwa mahojiano zaidi kuhusu ishu hiyo.
Ijumaa Wikienda: Je, ulitolewa posa lini?
Shishi: Hivi karibuni tu.
Ijumaa Wikienda: Kama hutaki kumwanika kwa maana ya picha lakini hata jina?
Shishi: Siwezi kuanika jina lake wala picha kwa sasa. Mashabiki wangu watamuona na kumfahamu siku ya harusi.Shishi Baby.

Ijumaa Wikienda: Je, harusi yenu itakuwa lini na itakuwaje?
Shishi: Mashabiki wangu wajue tu itakuwa soon na itakuwa ya aina yake kwani itafanyika uwanjani na mashabiki wataingia kwa kadi. Mchango utakuwa mdogo ili watu wengi zaidi wahudhurie.
Kabla ya kutolewa posa na mbali na wanaume wawili aliozaa nao, Shishi aliwahi kuripotiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na baadhi ya mastaa aliowazidi umri akiwemo Nuh Mziwanda, Hamadai na wengine.
NENO LA MHARIRI
Kinachoonekana Shishi ambaye ni mama wa watoto wawili wa kike aliozaa na wanaume tofauti, naye amechoka kupigwa na baridi na ukizingatia alishapita kwenye mikikimikiki mingi ya kimapenzi hivyo mashabiki wake wakae macho kodo kushuhudia harusi yake.
Ubuyu: Gladness Mallya |IJUMAA WIKIENDA| DarGet it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.