Header Ads

Kifo cha Bikira wa Kisukuma Kimegusa Wengi...Zamaradi Mketema Afunguka Mazito.....

Ikiwa bado Watanzania wapo kwenye majonzi mazito ya kuondokewa na Mtangazaji wa Kituo cha Radio EFM, Seth Katende maarufu kwa jina la Bikira wa Kisukuma aliyefariki dunia Jumapili ya Julai 9, 2017, watu maarufu nchini wakiwemo wasanii na watangazaji wameonyesha hisia za kuguswa na msiba huo.

Miongoni mwao, yupo mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds Tv, Zamaradi Mketema ambapo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika ujumbe ambao umegusa mioyo ya watu wengi na kuamsha simanzi kwa mashabiki wa Bikira wa Kisukuma, ujumbe wenyewe unasomeka hivi:

“Kuna WENGI lakini MUNGU ameamua kukuchukua wewe kwanza, AMEKUCHAGUA WEWE KWA SABABU, kupitia wale tunaowaamini na kuona kitu ndani yao MUNGU huamua kuonesha UKUBWA na utukufu wake, kupitia WEWE MUNGU ametuonesha ufalme wake, MUNGU ametukumbusha kuwa tunarudi kwake, MUNGU anataka tujue DUNIA NI YAKE, pamoja na sababu nyingi za kibinaadamu zinazoweza kutuonesha ulistahili kupewa muda kidogo lakini bado amekuchukua, AMEFANYA MAAMUZI MAGUMU, hakutaka kuangalia hata mtoto wako mdogo aliekuwa bado akikuhitaji, yeye haangalii hayo, na hili ni funzo kwetu, haangalia ni nani una nini ama una kipi hujatimiza, ikifika siku akikuita utaitika tu sababu lazima Dunia iendelee, leo umeondoka wewe kesho hatujui ni ya nani, MUNGU AMETENDA!! Safari yako umeimaliza Seth.

Kupitia mitandao nilianza kukujua kabla hatujafahamiana, na ni kutokana na kile alichokubariki nacho MUNGU, Na kama nilivyokujua kuna wengi uliweza kugusa maisha yao kwa namna moja ama nyingine, na hiyo ikakufanya ujulikane ndani ya muda mfupi, ulikuwa na NDOTO nyingi, ulikuwa na mipango mingi, na zaidi hata juhudi katika kufukuza ndoto zako, lakini MUNGU HAKUTAKA ZITIMIE, Leo UMELALA ukiwa hujatimiza nusu ya ndoto zako labda, huenda ulijua kesho itakuwepo utaamka, utapigana tena lakini MUNGU akasema hapana, muda umefika, na hata ungefanikiwa kuzitimiza leo pia bado nawaza na kujiuliza ukiwa umelala zingekusaidia vipi huko uendako ambako hakuna anaepajua kati yetu panafananaje, tukumbuke kuna KESHO, na kuitengeneza ni matendo yetu na kufata Dini zetu zinavyotaka, Dunia sio rafiki, na maamuzi ni yetu bado kuamua kuibeba au kuidharau.

Instagram imetikisika leo, na hiyo inaonesha ulikuwa ni nani na ulikuwa na mchango mkubwa kiasi gani, Seth Umeniumiza lakini umenifundisha kitu kikubwa sana, Kapumzike kaka.
.ALLAHU AKBAR!!

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.