Header Ads

Kisa Kusambaza Picha za Uchi za Mpenzi Wake...Rob Kardashian Kafanya Jambo Hili Kwa Familia yake

Kijana kutoka familia ya Kardashian, aliyekuwa akitoka kimapenzi na mwanamitindo Blac Chyna, Rob Kardashian ameipigia magoti familia yake kwa kuomba radhi kwa kitendo alichokifanya kwa mama mtoto wake.


Rob alifunguliwa mashitaka siku ya Jumatatu na mazazi mwezake  kwa kosa la  kumdhalilisha na kumyanyasa kijinsia kwa kuposti picha zake za utupu.

Chanzo cha karibu na familia kimeeleza kuwa Rob ameongea na dada zake pamoja na mama yake na kuwaomba radhi kwa kuposti picha yenye udhalilishaji katika mitandao ya kijamii. Pia mtu huyo ameeleza kuwa Rob anajutia kuweka hadharani malumbano yake na mwanamke huyo na hato fanya hivyo tena.

Hata hivyo baba  Dream hakuomba radhi kwa madai yaliotolewa ya kuwa alikuwa akimnyanyasa kijinsia Blac, bali alisema anajutia kupuuza ushauri aliopewa na dada zake juu ya kuto kuwa na mahusiano na mwanamke huyo.

Inaelezwa kuwa familia hiyo imemshamsamehe kijana huyo na ndio maana hawakusapoti alichokuwa akikifanya katika mitandao.

Na Laila Sue

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.