Header Ads

MTANZANIA Anayeigiza Kama 'YESU' Asimulia yanayomkuta

Msanii wa kuigiza Ayoub ambaye katika tamthilia ya 'Jambo na vijambo' anaigiza kama Yesu amefunguka na kusema kuigiza kama Yesu katika tamthilia hiyo inamletea shida kwa baadhi ya watu ambao siyo waelewa.

Ayoub alisema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha eNewz na kudai kuwa kuna wakati hata majirani waligombana na mkewe na hawakutaka kusemeshana naye kwa kuwa mumewe anamuuigiza 'Yesu'

"Hata mke wangu kishagombana na watu kwa sababu tu ya mimi kuigiza kama Yesu, wanamwambia mumewe anamgeza mtume wetu Yesu wetu kwa hiyo usinisemeshe, mke wangu akaja kunipa mimi hizo habari nikabaki kucheka tu, lakini katika ule u serious zaidi sijaona kama kumetokea tatizo kubwa mimi ni muislam lakini yapo makanisa yananiita nikawasaidie kutengeneza kazi ya sanaa baada ya kuniona kwenye kile kipindi, kwa hiyo wenyewe wakristo ambao wamezama kwenye imani kuniona naigiza kama Yesu hawafikirii vibaya sababu hata nachoigiza mle ndani kinaendana na yale aliyokuwa anatenda Yesu, hivyo huwezi kuona amefanya jambo lolote baya yule muhusika wa Yesu ambaye ni mimi" alisema Ayoub

Mbali na hilo Ayoub anasema watu ambao wanakuwa na mtazamo hasi juu ya uhusika wake kama Yesu ni wachache sana ukifananisha na wale ambao wanafurahia kwani mambo mengi ambayo anafanya muhusika ni mambo ya msingi.

"Hata ukiangalia kwenye ukurasa wa facebook wa EATV tukiweka post akitokea mtu ambaye atazungumza vibaya juu ya 'character' Yesu wapo watu wengine wanakuja kumsema sana na kumuelewesha vizuri juu ya uhusika wa Yesu, kwa hiyo utaona watu wanaozungumza uzuri wanashinda kutokana na mazuri ambayo muhusika amefanya" alisema Ayoub

Kipindi cha Jambo na Vijambo kinaruka kila Jumapili kuanzia saa 12:30 jioni katika ting'a namba moja kwa vijana EATV

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.