Header Ads

NJIA Anazotumia Mungu Kukujulisha Kuwa Mpenzi/Mchumba Uliye Nae si sahihi

Habari za jumapili ndugu wote.! ni siku nyingine ambayo Mungu ametupa nafasi ya kukutana hapa na kujulishana machache ambayo kwa hayo tunaweza kupiga hatua katika eneo hili la kimahusiano.

Kwanza kabisa ni lazima nikueleze ya kuwa sisi sote ni watoto wa Mungu na Mungu anatupenda sana..! ndio sababu akamtoa Yesu kwa ajili yetu.. (Yohana 3:16)

Mungu anapoona tunafanya maamuzi ambayo si sahihi au hayapo katika mapenzi yake huwa anatujulisha mapema sana ili tusiweze kupata madhara ya maamuzi yetu hapo baadae, na moja ya maamuzi hayo ni kuamua kuwa na mpenzi au mchumba. Je.! nitajuaje kama mchumba/mpenzi niliye nae ni sahihi au si sahihi? Zipo njia kadhaa ambazo Mungu huzitumia kukujulisha kuwa mchumba/mpenzi uliye nae si sahihi na hayo mahusiano yataishia pabaya au kuwapeleka jehanamu kabisa... Njia hizo ni kama hizi zifuatazo;

1. Huzuni moyoni (kujihukumu/kujilaumu moyoni)
Hii ni njia mojawapo muhimu sana ambayo Mungu huitumia kukujulisha kuwa mtu uliye naye si sahihi, unakuta tangu umeanza mahusiano na huyo mtu kuna hali ya huzuni moyoni mwako inaendelea na wakati mwingine unajisikia kujilaumu kwa nini nilimkubalia huyu mtu au kwa nini nilishawishika kutongoza huyu msichana, na wengine wameenda mbali zaidi wanaanza kubadilika kimatendo kwa wapenzi wao ili kudhihirisha kile kinachoendelea mioyoni mwao, hebu tuangalie maandiko haya katika Biblia;

2. Wakorintho 7:9 inasema “Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara… maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.”

Huyu ni Paulo anawaambia wakorintho kuwa huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu na lisilo na majuto.., kwa maana nyingine ukiona ndani yako unasikia huzuni au kujilaumu au kujihukumu juu ya huyo mpenzi wako basi ujue Mungu katika Roho mtakatifu anakuambia hivi.. "Fanya toba juu ya huyo mtu na uachane nae mara moja.!" la sivyo utapata hasara katika hayo mahusiano. Toba maana yake ni Repent (change your mindset) au badili msimamo wako juu ya huyo mtu. Mungu amekuletea hiyo huzuni moyoni kukujulisha kuwa utapata hasara juu ya mahusiano yenu na huyo mtu. Hata unaposoma haya maneno saivi na ukaona unajisikia hiyo hali ya kujihukumu inajitokeza basi ujue ni ishara Roho mtakatifu anakuthibitishia juu ya hili jambo ili ulifanyie kazi.


2. Njia ya Ndoto 
Hii ni njia nyingine ambayo Mungu huitumia kukujulisha kuwa mpenzi huyo uliye nae si sahihi na unahitaji kubadili msimamo wako. hebu tutazame maandiko haya katika Biblia;

Ayubu 33:14-15 inasema "Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, usingizi mzito huwajiliapo watu, katika usingizi kitandani."

Hapa nataka uone ya kuwa Mungu huwa anaongea na watu kwenye ndoto, mara ya kwanza, na anaweza kurudia mara ya pili lakini watu hawajali.. na ndio maana kuna ndoto nyingine unaota zinajirudiarudia lakini wewe hujali, ujue hufanyii kazi kile ambacho Mungu anakueleza katika ndoto, sasa hata katika mahusiano ni hivyo hivyo, kuna mambo ambayo huwa unaota juu ya mpenzi wako lakini wewe unayapuuzia na huyajali kumbe ni Mungu anakueleza juu ya huo uhusiano wenu ambao si mzuri, kwa mfano mtu anaota anakimbizwa na mpenzi wake, au anachomwa kisu na mpenzi wake au unagombana na mpenzi wako.. maana yake hiyo ni ishara Mungu anakupa kuwa huyo mtu si mzuri kwako na si mtu sahihi kwako, atakusababishia matatizo makubwa katika mahusiano yako, na wengine kwa kupuuzia huku wamejikuta wameingia kwenye matatizo makubwa na majuto makubwa wakati Mungu aliwaonyesha mapema katika ndoto.. mimi sijui huwa unaota ndoto gani juu ya huyo mpenzi wako au juu ya uhusiano wenu lakini naamini Mungu huwa anaongea na watu kwenye ndoto, hivyo uwe makini na ndoto unazoota juu ya mpenzi wako, sasa ukishaota hizo ndoto inakua rahisi kumueleza huyo mtu na kuamua kuachana la sivyo kile ulichokiona katika ndoto kitatokea...

Hizi ni baadhi ya njia chache ambazo Mungu huzitumia kukujulisha juu ya mahusiano yako na juu ya huyo mpenzi wako kama si sahihi kwako, lakini zipo njia nyingi mno! labda tukipata nafasi wakati mwingine tutashirikishana zaidi.

Mungu akubariki, na uwe na jumapili njema.!!

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.