Header Ads

Amber Lulu Kanasa Kwa Bwana Mpya....Adai Anampenda Hadi Anatamani Kujiteka........


Muuza nyago (video queen) ambaye hivi sasa amejitosa kwenye Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ ameamua kuwadorishia wenzake kwa kujishaua laivu na bwana’ke mpya.

Nusanusa ya Ijumaa Wikienda ilibaini kwamba, bwana huyo mpya wa Amber ni msanii wa Bongo Fleva anayekwenda kwa jina la Zulfika Hamisi ‘Jamwehe’ ambaye ilisemekana kwamba, ndiye aliyemshawishi mrembo huyo kufuta tatuu za mpenzi wake wa zamani, David Genz ‘Young D’.


Juu ya bwana’ke huyo mpya, Amber Lulu alilieleza Ijumaa Wikienda kuwa, sasa hivi ameamua kumuweka hadharani mpenzi wake bila kuhofia chochote kwani hata wale ‘nyakunyaku’ wa mabwana wa wenziye watagonga mwamba kwake.


Amber Lulu.
“Nampenda hadi natamani kujiteka, kiukweli hapa nimekufa hadi sijielewi. Ndiyo maana sioni aibu yoyote kujiachia naye na bado nitaonesha watu kuwa hata mimi najua kupenda,” alisema Amber Lulu anayekimbiza na ‘lijisongi’ lake la Watakoma.
Amber Lulu asiyeishiwa vimbwanga kama yule Amber Rose wa Marekani aliongeza kuwa, kwa sasa amejipanga kutulia tuli kwa jamaa huyo kwani ameona ni mwanaume mwenye malengo na mtazamo tofauti.

“Hapa mapepe yangu kwishnei kabisa na huwezi kuamini nipo tayari hata kwa ndoa,” alisema Amber Lulu. Kwa upande wake, jamaa huyo alifunguka kuwa, ana nia ya kweli na Amber Lulu na yupo tayari kwa lolote. “Ninampenda sana Amber (Lulu), ni mwanamke wa tofauti na wanavyomchukulia,” alisema Jamwehe.
Stori: Imelda Mtema, Dar

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.