Header Ads

Fid Q Azikana Team Kiba na Diamondi Achukizwa na Ommy Dimpozi


Fid Q Azikana Team Kiba na Diamondi Achukizwa na Ommy Dimpozi
Baada ya maneno kuwa mengi kuhusu ngoma yake ya Fresh Remix, Fid Q amefunguka na kusema hakujua kama mistari ya Diamond ilikuwa na lengo la kumdiss Alikiba kwa sababu yeye ni mtu wa hip hop na hajui chochote kuhusu Bongo Flava.

Rapper huyo ameeleza kuwa alikuja kujua hilo wakati wimbo umeshatoka hata hivyo hakuona kama kuna kibaya kilichofanyika kama inavyodai ila hajapendezwa na kitendo cha Ommy Dimpoz kuchukulia suala hilo binafsi zaidi na kuondoa maana ya burudani.

“Ok nyimbo imeshatoka na ndio imekuwaa hivyo nikaangali kama upande ule mwingine watasikia hii kitu na you know it entertainment industry, wataipokea kama biashara yenyewe ilivyo, huenda nao wakasema Fid na sisi tunataka hii beat because am cool both of side, mimi siyo tema Diamond, siyo team kiba nawapenda wote ningewagea beat,” amesema.

“Lakini niwe muwazi hiyo hope ilifutwa nilipokutana na post ya Ommy Dimpoz, kwamba ameweza kubadilisha ile burudani yote na kuipeleka katika kitu binafsi kabisa, imeniondolea lile vibe,” Fid Q ameiambia Clouds Tv.

Hata hivyo Fid Q ameongeza kuwa alichofanya Diamond siyo disrespect kwa Alikiba bali ni battle skills na siyo taarabu kwa watu wengi walivyokuwa wakidai katika mitandao.

“Hip hop majibizano yapo unakuwa unamgusia vitu vyako kwa kupitia muziki na msanii unashauriwa unapokuwa na ishu na mtu njia sahihi ya kuwasilisha ni kupitia muziki huo huo. Sitaki kusema Kiba alikosea kwa kujibu kwa tweet labda hakujisikia kuingia studio kufanya, yale ni maamuzi yake na menejiment yake hatuna budi kuyaheshimu,” amesema Fid.

Alipoulizwa mtazamo wake ni upi kuhusu beef ya Diamond na Alikiba, Fid alisema  kila mmoja ana team yake ya mtandaoni ambayo ipo imara ila kilichomkuta ni kuoga matusi kutoka kwa team Kiba.

“Kuna mtu aliniambia Fid umefanya ngoma na Diamond tengemea matusi kutoka kwa team Kiba ya online, nimeoga matusi sana ambayo sijawahi kuyaoga. Watu wamenidhalilisha sana, nasikitika kwamba nimevisoma lakini kujibu mtu siwezi kwa sababu wengi wamenihukumu katika vitu ambavyo si vyangu mwenyewe kwa hiyo nimeamua kuwaacha muda utazidi kuwaponya zaidi ,” amesisitiza.

Fresh Remix ni ngoma ya Fid Q ambayo amemshirikisha Diamond na Rayvanny, kutokana mistari ya Diamond kuonekana inamlenga Alikiba, naye alijibu kupitia mtandao wa twitter. Siku iliyofuata Diamond aliachia audio clip katika mtandao wa Instagram ambayo inaaminika ilimlenga Ommy Dimpoz na Alikiba, ndipo Dimpoz alipochua uamuzi wa kuandika maneno makali kwa Diamond na familia yake katika mtandao wa Instagram.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.