Header Ads

Hizi Hapa Faida 6 za Kuoa Mwanamke Kama Zari Hassan wa Diamond Platnumz

Mwanadada maarufu nchini Uganda, Zari Hassan, ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa na mzazi mwenza wa mwanamuziki Diamond Platnumz amekuwa akitajwa sana kwenye vyombo vya habari kuliko wanawake wengi, na mara nyingi kati ya hizo amekuwa akitajwa kwa ubaya.

Mwanadada huyu mwenye taswira ya utata amekuwa akitajwa kwenye vyombo vya habari vya nchini Uganda vikimuelezea kwa taswira kadhaa kama mrembo wa Uganda mwenye watoto watano, mtalaka wa milionea – Ivan Don Ssemwanga na sasa mzazi mwenza wa mmoja wa wanamuziki wanaolipwa pesa nyingi zaidi hapa Tanzania, Diamond Platnumz.

Shutuma nyingi anazopewa kwenye vyombo vya habari zimesababisha achukiwe na baadhi ya mashabiki zake na wakati huohuo kumuongezea mashabiki wapya wengi zaidi ya wanaomchukia. Japokuwa wengi, hasa mahasimu wake hawatakubali, Zari ni mwanamke ambaye kila mwanaume angependa kuwa naye.

Zifuatazo ni sababu 6 za kumfanya mwanaume atake kumuoa Zari wakati wowote:

1. Anajua kupika

Tunaanza na hili kwakuwa tofauti na wengi ambao wanaotengeneza kucha na kuosha mikono kwa bei ghali kama yeye wasingekubali kuingia jikoni kupika na badala yake wangetumua wafanyakazi wa ndani kwa ajili ya kazi hiyo. Mara mbili ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa jikoni akipika na hilo huwezi kuliona kwenye akaunti nyingi za ‘wanawake wa mjini.’

2. Ana uhusiano mzuri sana na wanae

Ingawa inaonekana anapitia mengi akiwa na mzazi mwenzie (Diamond), Zari amekuwa na uhusiano mzuri sana kati yake na watoto wake. Muda mwingi anakuwa nao na moja kati ya nyakati zilizodhihirisha hili ni katika mazishi ya mtalaka wake, Ivan. Hata wakati ambao Diamond alikuwa hajafika, alibaki kuwa imara kwa ajili ya wanae wakubwa.

3. Tukiongelea uimara alionao, tazama jinsi anavyokabiliana na maneno mengi yanayosemwa na mahasimu wa mapenzi kati yake na Diamond Platnumz

Hakumshambulia wala kumkosoa mpenzi wake huyo Diamond aliposema kwamba huwa anamtafuta akiwa na hamu ya kufanya mapenzi kwakuwa Zari si muaminifu. Pamoja na utoto huu aliofanya Diamond, ambao bila shaka Zari haupendi, bado ameweza kumsamehe na kuendelea maisha yao ya pamoja.
Kwa wengi, hili halikuchukuliwa kama ni uamuzi wa busara uliofanywa na mwanamke huyo, bali lilitafsiriwa kama anang’ang’ania mapenzi na Diamond, hata kama ananyanyaswa. Mbali na tafsiri zote zitazotolewa na mashabiki, uwezo wa mwanamke kusamehe jambo kama hilo kutoka kwa baba wa wanae linaonesha ungangari wa hali ya juu kabisa, hasa ukizingatia kwamba mambo mengi maishani mwake yalikuwa yanamuendea kombo, ikiwemo kifo cha mtalaka wake mwezi Mei.

4. Anajiweka kwenye mvuto wa hali ya juu siku zote, muda wote

Akiwa na umri wa miaka 35 na watoto watano, Zari bado ana muonekano wa kuvutia sana kana kwamba ni binti wa miaka ishirini. Amekuwa akiwatoa udenda wanaume wengi akiposti picha akiwa amevaa kivazi cha kuogelea kinachoweka wazi maumbile yake akiwa mapumzikoni, ikiwemo ya hivi karibuni alipokuwa mapumzikoni jijini Mombasa na mpenzi wake Diamond. Anafanya mazoezi, anakula vyakula sahihi na pia anawaambia mashabiki zake wa Instagram siri za urembo wake. Tuweke kando nguo za bei ghali anazovaa.

5. Kuhusu watoto, hajali kuhusu kujiwekea idadi wala uzazi wa mpango

Ukiacha watu maarufu nchini Kenya kama Julie Gichuru mwenye watoto wanne na Akothee mwenye watoto watano, Zari ni mtu pekee maarufu anayejulikana kwa kuzaa watoto wengi kwa urahisi. Kwa kuangalia picha zake tu, mtu yeyote anaweza kukubali kwamba Zari anapenda kuwa mama na jambo hilo ni nadra sana kulipata kwa wanawake kwenye tasnia ya sanaa na burudani.


6. Anaweza kusimamia vizuri biashara na miradi ya familia

Zari hapati tabu kabisa kubadili muonekano wake wa mvuto wa kimapenzi na kuvaa suti kuwa tayari kibiashara. Mtalaka wake Ivan Don alipofariki, Zari amepewa mamlaka yote kuhusu usimamizi wa mali za watoto wake na ameachiwa kuendesha biashara nyingi ambazo walikuwa wakizifanya kwa ubia. Kwa upande mwingine, Zari ameshaanza kuwekeza kwa ajili ya watoto wake wadogo kwani mpaka sasa mtoto wa mwisho ni balozi wa kampuni ya nguo za watoto. the difference:  Zari is one of the few who chose not to let them define her

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.