Header Ads

Madai ya Mwanamuziki Nandy Kudaiwa Kuchukua Nafasi ya Ruby.."Ruby Afungukia Nandy"

Madai ya Mwanamuziki Nandy Kudaiwa Kuchukua Nafasi ya Ruby.."Ruby Afungukia Nandy"
Msanii wa muziki Bongo, Ruby amesema hawezi kumchukia msanii mwezake Nandy ambaye watu wamekuwa wakidai amechukua nafasi yake kwenye muziki.

Hitmaker huyo wa ‘Na Yule’ amedai maneno ya watu hayawezi kumfanya akamchukia Nandy au kuonea wivu mafanikio wake bali anafurahi pia anapoona anafanikiwa zaidi.

“Kwanza siwezi nikamchukia Nandy kwa sababu watu kama hawajui sisi tumeshafanya kazi, kuna wimbo kipindi nipo THT unaitwa Mama ya Butterfly Group, tupo mimi Nandy, Maua Sama na Alice, kwa hiyo siwezi nikamchukia kwa sababu anafanikiwa,” Ruby ameiambia FNL ya EATV na kuongeza.

“Furaha yangu ni kuona anafanikiwa maisha yake yote kwa sababu ni mtu nimeshafanya naye kazi mara kibao, tumeshakutana mara kibao studio. Kwa hiyo mimi naona hizi rumors za watu zinazoendelea out site sijui kachukua nafasi yangu ni maneno ya watu ambayo yapo kila kukicha lakini hayawezi kunigusa mimi nimchukie Nandy na siwezi nikajifaninisha naye,” amesisitiza Nandy.

Msanii wa Nay wa Mitego katika wimbo wake uitwao Moto kuna mistari anatamka kuwa pengo la Ruby ni Nandy kitu ambacho kimekuwa kikizungumzwa mtaani na mitandaoni.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.