Header Ads

Madhara ya Kutumia Vidonge vya Uzazi wa Mpango Kwa Wanawake


Ili kuepuka kupata ujauzito, wanawake hutumia njia mbalimbali za kupanga uzazi wao ikiwa ni pamoja na utumiaji wa vidonge, vitanzi, vijiti na wengine hutumia mipira wakati wa tendo la ndoa.

Njia hizi kila moja ina athari chanya na hasi na mara nyingi hutegemea na hali ya mtu anayezitumia kwani akitumia mmoja anaweza kuona madhara kadhaa lakini mwingine asione.

Katika kuchambua madharaya ya njia hizi za kupanga uzazi, tutaelezea madhara ya matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa wanawake.

Kupata kichefuchefu.

Mtumiaji anayetumia dawa hizi kwa mara ya kwanza ana uwezekano mkubwa wa kupatwa na kichefu chefu ambacho hudumu kwa muda mfupi hadi mwili utakapozoea dawa hizo. Ukitumia dawa hizi wakati wa chakula, au muda mfupi kabla ya kulala huenda ikakusaidia kupunguza hali hiyo.

Aidha, unashauriwa kuwa, endapo utaona hali hiyo imeendelea kwa muda mrefu, muone mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi.

Kuongeza hamu ya kula

Wakati mfumo wa homoni za oestrogen na progesterone unapobadilishwa kwa kutumia vidonge humfanya mtumiaji kuwa na njaa sana na hivyo kukufanya ule sana hali inayoweza kupelekea kuongezeka uzito. Lakini hakuna ushahidi madhubuti unaoonyesha uhusiano wa moja kwa moja kuwa dawa hizo zenyewe huongeza uzito.

Kubadilika kwa hisia (moody)

Wanawake ambao hukumbwa na matatizo ya kubalika kwa hali/hisia zao kama kuwa na hasira, kutotaka kusemeshwa, hali hiyo huongezeka pale anapotumia vidonge vya kupanga uzazi. Wanawake wa aina hii wanashauriwa kujadiliana na wenza wao kabla ya kuanza kutumia dawa hizi.

Maumivu ya kichwa

Mabadiliko ya homoni katika mwili wa mwanamke anayetumia vidonge hivi, hupelekea maumivu ya kichwa na kipandauso. Mabadiliko tofauti ya homoni hupelekea dalili tofauti tofauti za maumivu ya kichwa. Lakini maumivu na dalili hizo zitaendelea kupungua kadiri ya muda.

Kuganda wa damu

Mtumizi ya vidonge hivi wakati mwingine huwaweka wanawake katika hatari kubwa kutokana na kupelekea damu zao kuwa mabonge mabonge. Wanawake wenye matatizo haya ya damu kuwa mabonge wanashauriwa kutotumia dawa hizi kwani zitawasababishia madhara zaidi. Lakini pia kabla hujaanza kutumia dawa, unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya.

Maziwa kuongezeka ukubwa

Vidonge hivi vinaweza kukusababishia maziwa yako kuongezeka ukubwa au kupata maumivu ya maziwa madhara ambayo yataanza kutoonekana baada ya kutumia dawa hizi kwa wiki kadhaa. Hata hivyo, kama utaona maziwa yako hayapo sawa, au maumivu yamedumu kwa muda mrefu, utahitaji kumuona mtaalamu wa afya haraka.

Kutokwa na uchafu ukeni

Baadhi ya wanawake hukumbwa na tatizo la mabadiliko ya utoaji uchafu ukeni hali ambayo huathiri kujamiiana kwao kutokana na kupungua au kuongezeka kwa muda na kiasi cha utoaji uchafu. Utoaji wa uchafu kwa njia ya uke si tatizo kwa wanawake, lakini kama utahisi kuna hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda hospitali.

Athari hizo za vidonge tulizozitaja hap juu sio zote ni mbaya. Madhara mengine kubwa za kutumia vidonge hivyo ni pamoja na kuumwa sana na kichwa, Maumivu ya nyonga, maumivu ya kifua, uono hafifu pamoja na maumivu ya miguu au mapaja.

Endapo moja ya haya madhara makubwa tuliyoyataja hapo yatatokea, unatakiwa kumuona daktari haraka ikiambatana na kusitisha matumizi ya videonge hivyo.

Maumivu hayo yanaweza kuashiria matatizo katika kibofu, ini, damu kuwa mabonge, shinikizo la damu au hata ugonjwa wa moyo.

Chanzo: The Citizen

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.